Thursday , 2 February 2023
Home Gazeti Habari za Siasa TCD yaomba mabadiliko Sheria Vyama vya Siasa kufikia Julai
Habari za SiasaTangulizi

TCD yaomba mabadiliko Sheria Vyama vya Siasa kufikia Julai

Zitto Kabwe, Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD)
Spread the love

 

MWENYEKITI wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD), Zitto Kabwe ameiomba Serikali kuhakikisha mabadiliko ya Sheria ya Vyama vya Siasa yanafanyika kufikia Julai mwaka huu ikiwa ni maadhimisho ya miaka 30 ya mfumo wa vyama vingi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Zitto ambaye pia ni Kiongozi wa ACT-Wazalendo ametoa ombi hilo jijini Dodoma leo Jumanne tarehe 5 Aprili 2022 kwenye mkutano wa kitaifa wa maridhiano, haki na amani ulioandaliwa na kituo hicho.

“Kama itakupendeza Mh. Rais (Rais SamiaSuluhu Hassan) na kama taratibu za Serikali zitakuwa zimekamilika tutafurahi tutakapokuwa tunaadhimisha miaka 30 ya mfumo wa yma vingi tuwe tumefanya maboresho ya Sheria ya Vyama vya Siasa,” amesema Zitto.

Pia Zitto ameimba Serikali kuendelea kutekeleza mkataba wa kutoa ruzuku kwa TCD walioingia katika Serikali ya awamu ya nne.

Amesema TCD iliingia makubaliano na Serikali ya awamu ya nne ya kupokea ruzuku kwaajili ya kusaidia uendeshaji wa kituo hicho ambacho alisema kazi yake kubwa ni kuponya majeraha baada ya kila uchaguzi kwa majadiliano na maridhiano.

Hata hivyo alisema kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wao, TCD haikuweza kufanya mikutano ya maridhiano baada ya uchaguzi wa mwaka 2015 na ule wa 2020, lakini hakueleza ni sababu zipi hasa.

Zitto amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuonesha nia ya maridhiano tangu aliposhiriki mkutano wa wadau wa siasa ya demokrasia ya vyama vingi ambao ulitoka na maazimio ambayo yameanza kuboresha mazingira ya ufanyaji siasa.

Akijibu maombi hayo Rais Samia amesema suala la kurudisha ruzuku kwa mwaka wa fedha ujao limeshachelewa kwani makadirio ya bajeti yameshafungwa “ lakini ni suala linalojadilika.”

Kuhusu maboreshi ya Sheria ya Vyama vya Siasa kabla ya Julai mwaka huu alisema inategemea na majadilinao yatakavyokuwa.

“Kama yatakuwa controversial inabidi tukutane mara kwa mara na muda unaweza usitoshe lakini kama yatakuja kwetu yakiwa vizuri sisi hatuna shida yatafanyika ili tuseme tumesboresha Sheria yetu baada ya miaka 30,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Kamati ya Bunge yaitaka Serikali ichukue hatua kudhibiti mfumuko wa bei

Spread the love  SERIKALI ya Tanzania imetakiwa kufanya tathimini dhidi ya changamoto...

Habari za Siasa

Bunge lataja kinachokwamisha Mradi wa Mchuchuma na Liganga

Spread the love  MRADI wa uchimbaji chuma cha Liganga na Makaa ya...

Habari za Siasa

Chongolo aagiza watendaji wanaoonyesha mianya ya rushwa wakamatwe

Spread the love   KATIBU mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa...

Habari za Siasa

TRA iweke mfumo wa msamaha wa kodi kutekeleza miradi

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Taifa kimeitaka Mamlaka ya Mapato...

error: Content is protected !!