Friday , 3 February 2023
Home Gazeti Habari Maofisa Ughani kumilikishwa pikipiki baada ya miaka miwili
Habari

Maofisa Ughani kumilikishwa pikipiki baada ya miaka miwili

Spread the love

MAOFISA Ughani nchini watamilikishwa pikipiki zinazotolewa na Serikali baada ya kuzitumia kwa miaka miwili katika kutoa huduma kwa wakulima. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Hatua hiyo inakuja baada ya Rais Samia Suluhu Hassan leo Jumatatu tarehe 4 Aprili 2022 kuridhia ombi lilotolewa na Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe.

Awali Bashe alisema Serikali haiwezi kushindwa kununua pikipiki hizo kila baada ya miaka miwili hivyo ni vyema wakamilikishwa ili zinunuliwezingine.

Serikali imegawa jumla pikipiki 7000 kwa maofisa ughani ambapo leo Rais Samia amegawa pikipiki 6,700 na zingine 300 zilishatolewa.

Hata hivyo Rais Samia amesema pikipiki hizo zitamilikishwa tu kwa wale ambao wataonekana wametekeleza majukumu yao ipasavyo.

“Haitakuwa blanked kwamba tutawamilikisha, hapana. Tutapima kwa kazi mnazofanya, na tunaamni kwa kipindi hicho thamani ya kazi yenu itakuwa imezidi hiyo ya pikipiki” amesema Rais Samia.

Ameongeza kuwa hatua hiyo itawapa hari ya kufanya kazi na kuzitunza pikipiki hizo wakijua baada ya hapo watazimiliki wao.

Mbali na pikipiki pia Rais Samia amesema Serikali itagawa vipima udongo kwa halmashauri 143, kutoa simu janja pamoja na visanduku 3300 kwa maafisa ughani.

Ametumia fursa hiyokuwataka maofisa ughani kutumia vitendeakazi hivyokama ilivyokusudiwa kwa manufaa ya Taifa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

HabariHabari Mchanganyiko

CRB yashtukia makandarasi wanaofanya ubia wa ujanja ujanja, yasema watakaobainika kuchukuliwa hatua kali

Spread the love  BODI ya Usajili wa Makandarasi (CRB), imeonya makandarasi wanaofanya...

HabariKimataifa

Aliyesomeshwa na mchumba aamuriwa kurudisha Sh 9.4 Mil. baada ya kukataa kuolewa

Spread the love  MWANAMKE mmoja nchini Uganda ambaye aliuumiza moyo wa mchumba...

Habari

Mnyika aacha ujumbe msibani kwa kada wa Chadema aliyefia vitani Ukraine

Spread the loveKATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo-Chadema Taifa, John...

HabariHabari Mchanganyiko

Mwili wa kada wa Chadema aliyefia vitani Ukraine wawasili, kuzikwa Mbeya

Spread the loveMWILI wa Kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo-Chadema, aliyefia...

error: Content is protected !!