Thursday , 2 May 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Marekani yaweka vikwazo kwa maafisa Somalia kwa kuchelewesha Uchaguzi
Kimataifa

Marekani yaweka vikwazo kwa maafisa Somalia kwa kuchelewesha Uchaguzi

Bendera ya Marekani
Spread the love

 

NCHINI Marekani kumeongezeka idadi kubwa ya maafisa wa Somalia , waliowekewa vikwazo vya usafiri kwa kuhujumu mchakato wa kidemokrasia nchini humo . Anaripoti Mwandishi Wetu [endelea ]…

Hayo yamejiri leo Alhamisi tarehe 17 machi 2022 baada ya Somali kukosa tena mkataba wa machi 15 ya kukamilisha uchaguzi wa Bunge ambalo limecheleweshwa kwa Zaidi ya mwaka mmoja .

Hata hivyo Majina ya Viongozi hao bado hayajatolewa .

Uchaguzi huo umesogezwa mbele hadi mwisho wa mwezi huu ili kuruhusu viti vilivyosalia katika Bunge la chini kabisa kujazwa .

Aidha Ubalozi wa Marekani nchini Somalia umepongeza majimbo ya Kusini Magharibi na Galmudug ,kwa kukamilisha uchaguzi wao wa Bunge kabla ya muda uliowekwa na kuelezeka kusikitishwa na ucheleweshwaji wa shughuli hiyo katika majimbo mengine .

Marekani inasema kuwa itatumia vikwazo vya usafiri , na zana zingine ilikukuza uwajibikaji na kuunga mkono kuhitimishwa kwa mchakato wa uchaguzi .

Taarifa hiyo ilibainisha kuwa kuna taarifa za kuaminika za ukiukaji wa taratibu ,unyanyasaji na vitisho dhidi ya waandishi wa habari na wanachama wa upinzani

Nchi ya Somalia haijafanya Uchaguzi unaohusisha wananchi moja kwa moja .

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifa

Mwanamke Rwanda ataka kupambana tena na Kagame

Spread the loveKIONGOZI wa kihistoria wa upinzani nchini Rwanda, Victoire Ingabire Umuhoza,...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

error: Content is protected !!