Friday , 3 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Wawili kuchuana uenyekiti ACT-Wazalendo Vijana Dar es Salaam
Habari za Siasa

Wawili kuchuana uenyekiti ACT-Wazalendo Vijana Dar es Salaam

Spread the love

NGOME ya Vijana ya Chama cha ACT-Wazalendo, Mkoa wa Dar es Salaam, kesho Jumapili, tarehe 13 Machi 2022, kinatarajia kufanya uchaguzi wa kujaza nafasi zilizowazi baada ya uongozi wake kuvunjwa. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Taarifa hiyo imetolewa jana tarehe 12 Machi 2022 na Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Ngome ya Vijana ACT-Wazalendo, Wakili Victor Kweka akitaja majina ya wagombea nafasi mbalimbali yaliyopitishwa na Sekretarieti ya Ngome ya Vijana ya chama hicho Taifa.

“Sektretarieti ya Ngome ya Vijana Taifa imepitisha wagombea 11 kati ya wagombea 12 waliochukua na kurejesha fomu, kwa nafasi saba zinazogombania,” imesema taarufa ya Wakili Kweka.

Taarifa ya Wakili Kweka imesema, katika uchaguzi wa nafasi ya Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana ACT-Wazalendo Mkoa wa Dar es Salaam, wamepitishwa watu wawili kugombea ambao ni, Felex Ferdinand Kamgisha na Rahim Yazidi Twaibu.

Katika nafasi ya katibu wa ngome hiyo, waliopitishwa kugombea ni Mwantum Ramadhani Gogo, Salumu Saidi Mkwanda na Shabani Selemani Kabena, huku nafasi ya katibu wa mipango na uchaguzi wakipitishwa Ally Justine Ng’wihend na Hamidy Mmanga Omary, kugombea.

Taarifa ya Wakili Kweka imesema, Mohammed Hassan Saidi, amepitishwa kugombea nafasi ya Katibu wa Habari, Uenezi, Mawasiliano na Umma wa ngome hiyo, wakati Hawa Omary Marock, akiteuliwa kugombea nafasi ya Mweka Hazina.

Katika nafasi ya mjumbe mmoja mwanamke wa Kamati ya uongoziya ngome hiyo, ameteuliwa Salma Khatibu Rashid kugombea, huku upande wa mjumbe mmoja mwanaume wa kamati hiyo akipitishwa Kassim Salum Mtigile kugombea.

Taarifa ya Wakili Kweka imesema, leo Jumamosi kutakuwa na mdahalo kwa wagombea nafasi ya uenyekiti wa ngome hiyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza uchaguzi mdogo Jimbo la Kwahani

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi, imetangaza uchaguzi mdogo...

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!