Friday , 26 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Meja Jenerali Urusi adaiwa kuuawa, Ukraine washangilia
Habari Mchanganyiko

Meja Jenerali Urusi adaiwa kuuawa, Ukraine washangilia

Spread the love

MAOFISA wa nchi za Magharibi pamoja Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ukraine, Anton Gerashchenko wamedai kuwa jenerali mwingine mwandamizi wa tatu ndani ya Jeshi la Urusi ameuawa nchini Ukraine. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Taarifa zinasema Jenerali Andrei Kolesnikov aliyetoka katika wilaya ya kijeshi ya mashariki mwa Urusi, ndiye aliyeuawa.

Kupitia akaunti yake ya Twitter Waziri huyo wa mambo ya ndani, amesema ni furaha iliyoje kuthibitisha kuwa Meja Jenerali watatu ameuawa katika mapambano hayo.

Awali jeshi la Ukraine lilisema Meja Jenerali Kolesnikov ambaye ni Kamanda wa jeshi la 29 la wilaya ya mashariki mwa Urusi, aliuawa.

Wachambuzi wa masuala ya kimataifa wamesema uwepo wa viongozi wa ngazi ya juu wa kijeshi ndani au karibu na uwanja wa vita inaweza kuwa ishara kwamba operesheni za Urusi haziendi kama zilivyopangwa.

Mbali na Kamanda huyo, Meja Jenerali mwingine ambaye anaingia katika kundi la viongozi wa ngazi za juu jeshini kuuawa ni Andrei Sukhovetsky aliyeuawa tarehe 2 Machi mwaka huu na kifo chake kuthibitishwa na Rais wa Urusi, Vladimir Putin.

Katika vita hiyo iliyoanza tarehe 24 Februari, mwaka huu inaelezwa kuwa wanajeshi kati ya 2000 hadi 4000 wa Urusi wameuawa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!