Saturday , 20 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Vijana 300 wapigwa msasa anuani za makazi Dodoma
Habari Mchanganyiko

Vijana 300 wapigwa msasa anuani za makazi Dodoma

Spread the love

VIJANA zaidi ya 300 walioajiriwa kwa ajili ya kubandika vibao vya namba za anuani za makazi katika jiji la Dodoma wamepatiwa mafunzo juu ya ubandikaji wa namba hizo katika nyumba. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma…(endelea).

Akizungumzia kuhusu mafunzo hayo Mratibu wa mradi wa anuani za makazi katika jiji la Dodoma, Joseph Nkuba amesema lengo ni kuhakikisha kazi inafanyika kwa ueledi na ufanisi.

Nkuba amesema katika jiji la Dodoma kuna kata 41 na mitaa 222 ambapo zoezi hilo linatakiwa kufanyika kwa ufanisi na kumaliza kwa wakati.

“Kutokana na umuhimu wa zoezi hili kikundi cha watu 100 watakuwa wakivamia kata moja na kuanza kubandika vibao vya namba za anuani za makazi na kwa ushirikiano huo kuna uhakika kuwa kwa siku kata tatu zitakuwa zikihudumiwa.

“Katika zoezi ambalo ni agizo la Rais Samia Suluhu Hassan tunategemea kulifanya kwa umakini mkubwa kwa kuzingatia zaidi umuhimu wa anuani za makazi na faida zake” amesema Nkuba.

Kwa upande Ofisa habari wa halmashauri ya Jiji la Dodoma, Ramadhani Juma amesema zoezi la ubandikaji wa anuani za makazi utaanza rasmi Machi 15 mwaka huu.

Juma amesema zoezi hilo litaanza katika kata ya Mtumba ambako kuna mji wa kiserikali.

Aidha, ametoa wito kwa wakazi wote wa jiji la Dodoma kuhakikisha wanatoa ushirikiano kwa wataalamu watakaokuwa wameambatana na wabandikaji wa vibao vya anuani za makazi.

Pia amewashauri wamiliki wa maeneo kuhakikisha au nyumba kutoa taarifa muhimu kwa wataalamu ambao wanahusika na ufanyaji wa zoezi.

“Zoezi hili linatarajiwa kumalizika Mei mwaka huu kwa hio ni litachukua siku zisizozidi 45,” amesema Juma.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wauguzi, madaktari 1000 kugawiwa mitungi ya Oryx Gas

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gas na Taasisi ya Doris Mollel Foundation...

Habari Mchanganyiko

Tanzania yachaguliwa Makamu wa Rais Tume ya Shirika la Hali ya Hewa Duniani

Spread the love  TANZANIA kupitia Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)...

Habari Mchanganyiko

NEMC yaonya wanaojenga bila tathmini ya mazingira

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC),...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

error: Content is protected !!