Sunday , 5 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Vigogo ACT-Wazalendo kurejea CUF
Habari za SiasaTangulizi

Vigogo ACT-Wazalendo kurejea CUF

Zitto Kabwe, Kiongozi wa ACT Wazalendo
Spread the love

 

BAADHI ya vigogo na wanachama wa Chama cha ACT-Wazalendo, wanaodaiwa kutoridhika na mchakato wa uchaguzi wa mwenyekiti wa chama hicho, wako mbioni kurejea Chama cha Wananchi (CUF). Anaripoti Regina Mkonde, Dar ea Salaam … (endelea).

Hayo yamesemwa leo Ijumaa, tarehe 4 Februari 2022 na Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mahusiano na Umma CUF, Mhandisi Mohamed Ngulangwa akizungumza na MwanaHALISI Online.

Amesema wanachama hao wa ACT- Wazalendo, walioshusha tanga kwenye chama chake wakati wa mgogoro wa kiuongozi kati ya aliyekuwa Katibu Mkuu, Maalim Seif Sharif Hamad na Mwenyekiti, Prof. Ibrahim Lipumba, wanatarajia kurejea kwa makundi matatu.

Amesema, kundi la kwanza litapokelewa kesho Jumamosi, tarehe 5 Februari 2022 na Prof. Lipumba, katika makao makuu ya CUF, yaliyopo Buguruni jijini Dar es Salaam.

Alipoulizwa majina ya viongozi watakaorejea CUF, Mhandisi Ngulangwa amekataa kutaja majina yao hadi kesho.

“Tumesema hivi, ili kutia uzito wa jambo lenyewe hatuwezi kuweka hadharani lakini ni watu wanaorejea ni wazito na kama nilivyoandika andiko langu hiyo ni awamu ya kwanza, maana kuna awamu tatu ya watu wazito na hizi awamu zitatofautiana ukubwa,” amesema Mhandisi Ngulangwa.

Mhandisi Mohammed Ngulangwa, Mkurugenzi wa Habari -CUF

Mhandisi Ngulangwa amesema “watakaokuja kesho kuna jambo litatokea katika siku mbili tatu Dar es Salaam na Zanzibar, kwamba maji yakipwa kuna muda inabidi yajae. CUF ni bahari inakupwa na kujaa, sifa yake kutoacha uchafu.”

Aidha, Mhanidisi Ngulangwa amesema katiia kundi hilo, wapo wanachama kutoka vyama vingine.

“Tutawapokea wanaotoka vyama mbalimbali, ndiyo maana tunasema walipoondoka kwa tanga na wanarudi kwa anga. Walishusha tanga, wakapandisha tanga huo ni usafiri duni sasa tunawarudisha kwa anga,” amesema Mhandisi Ngulangwa.

Mhandisi Ngulangwa amedai kuwa, sababu za wanachama hao kurejea CUF ni kutorudhushwa na uchaguzi huo uliomteua Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo, Juma Dunu Haji.

Juma Duni Haji

“Kuna mabaya makubwa yametokea kwenye uchaguzi wa ACT-Wazalendo wa tarehe 29 Januari 2022, si mambo ya kuzungumza hasa kwa sisi wapinzani wenyewe kuzungumzia yanatuchafua. Kule kumeoenaka kuna unafiki mkubwa hakuna siasa ya nia ya dhati ya kuiondoa CCM madarakani bali kutafuta ruzuku,” amedai Mhandisi Ngulangwa na kuongeza:

“Ukimuona mtu yupo kwenye siasa hizi pamoja na malengo kuwa tofauti lakini lengo kuu ni kuhakikisha haki inapatikana. Hasa aliyewahi kuwa CUF chama kinachohubiri haki, ukiona katoka kwenye chama alichokuwepo ni katika jitihada za kutafuta haki. Akiona gizani mahali inabidi arudi kwenye haki.”

Miongoni mwa watu wanaotajwa kurejea CUF ni aliyekuwa Afisa wa ACT-Wazalendo, Anderson Ndambo, ambaye hivi karibubi alitangaza kujivua unachama wa chama hicho akidai uchaguzi huo haukuwa wa haki.

MwanaHALISI Online ili mtafuta kwa simu Ndambo na kumuuliza juu ya swala hilo lakini hakujibu.

Mtandao huu pia ulimtafuta Katibu wa Itikadi na Uenezi ACT-Wazalendo, Janeth Rithe ilikupata ufafanuzi wa tuhuma hizo, ambaye amesema si za kweli kwani uchaguzi ulikuwa huru, wa haki na uwazi.

Prof. Ibrahim Lipumba, Mwenyekiti wa CUF

“Kuhama chama ni jambo la kawaida kwa wanasiasa hasa wanapoona pale walipo hawawezi kutumika tena,” amesema Rithe na kuongeza:

“Uchaguzi ulikuwa huru na haki na wa uwazi, kama waliona hakuna uhalali walipaswa wakate rufaa.Tuhuma za uchaguzi kuwa sio halali hizi sio za kweli unapoingia kwenye uchaguzi na mtazamo wa kushinda tu haya ndio madhara yake ukweli ni kwamba uchaguzi ni halali kabisa,” amesema

ACT-Wazalendo ilifanya mkutano mkuu maalum tarehe 29 Januari 2022 ambapo ilimchagua Juma Duni Haji maarufu Babu Duni kuchukua nafasi ya Maalim Seif ambaye alifariki dunia 17 Februari 2021, Hospitali ya Taifa ya Muhimbili akipatiwa matibabu.

Babu Duni alimbwaga mshindani wake wa karibu, Hamad Masoud Hamad.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Kimbunga Hidaya chatikisa Mafia

Spread the loveWAKATI hali ya upepo mkali ikiendelea kushuhudiwa katika baadhi ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mbatia ambwaga Selasini, mahakama yaamuru alipwe fidia

Spread the loveMAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, imemuamuru...

Habari za SiasaTangulizi

Mkulo afariki dunia, kuzikwa kesho Kilosa

Spread the loveALIYEKUWA Waziri wa Fedha na Mbunge wa Kilosa (CCM), Mustafa...

Habari MchanganyikoTangulizi

Usafiri baharini wasitishwa kukwepa athari za kimbunga Hidaya

Spread the loveUSAFIRI wa baharini umesimamishwa kwa muda ili kukwepa athari za...

error: Content is protected !!