Spread the love

 

WAKILI maarufu Alute Mughwai Lissu, kaka wa kiongozi wa chama cha siasa cha upinzani Tanzania cha Chadema, Tundu Lissu ametambulishwa mahakamani kama mgeni wa heshima wa upande wa utetezi katika kesi ya ugaidi inayomkabili Freeman Mbowe na wenzake watatu. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Alute ambaye makazi yake yapo jijini Arusha ni miongoni mwa waliojitokeza leo Ijumaa, tarehe 4 Februari 2022, Mahakama Kuu, Divisheni ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, Dar es Salaam kusikiliza mwenendo wa kesi hiyo mbele ya Jaji Joachim Tiganga.

Mara baada ya Jaji Tiganga kuingia, mawakili wa Jamhuri kutambulisha jopo la mawakili wote, upande wa utetezi unaoongozwa na Peter Kibatala naye ametambulisha mawakili wenzake.

“Kwa nafasi ya pekee naomba kumtambulisha Wakili Alute Mugwai Lissu, pamoja kwamba hayupo katika kolamu yetu, lakini ni mgeni wetu wa pekee leo,” amesema Kibatala

Baada ya Kibatala kumtambulisha, Wakili Alute akasema “Mheshimiwa Jaji kwa nafasi ya pekee nashukuru kuwepo mahala hapa na kusikiliza shauri hili.”

Kisha Jaji Tiganga aksema “karibu sana.”

Mbali na Mbowe kwenye kesi hiyo washtakiwa wengine ni, Adam Kasekwa, Mohamed Ling’wenya na Halfan Bwire ambao walikuwa makomandoo wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

Kwa sasa shahidi wa 13 wa Jamhuri, Tumaini Sostenes Swila (46) anaendelea kutoa ushahidi wake mahakamani hapo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *