Wednesday , 8 May 2024
Home Kitengo Biashara Nyumba 50 ndani ya jengo la Uhuru Heights kuuzwa
Biashara

Nyumba 50 ndani ya jengo la Uhuru Heights kuuzwa

Spread the love

Kampuni ya Cosmos Properties ya jijini Dar es Salaam, ambayo ni mmiliki wa nyumba 50 katika jengo la Uhuru Heights iko matatani baada ya nyumba hizo kutolewa notisi ya kuuzwa ili kufidia deni linalotokana na mkopo wa benki ya Exim. Anaripoti Mwandishi Wetu… (endelea).

Mdaiwa huyo aligomea kuiruhusu kampuni ya uwakili ya Hallmark Attorneys iliyopewa nguvu ya kisheria na benki hiyo kusimamia mali hizo kutekeleza agizo hilo.

Tukio la Mdaiwa huyo kugomea uamuzi huo wa kisheria limetokea mwanzoni mwa wiki hii jijini Dar es Salaam mara baada ya maofisa wa kampuni ya uwakili ya Hallmark Attorneys kufika kwenye jengo la Uhuru Heights kufanya ukaguzi wa kutathmini mali hizo, ambapo licha ya mdaiwa huyo kuonyeshwa nyaraka zote muhimu ikiwemo hati ya taarifa ya utekelezaji wa amri bado aligoma kutii agizo hilo.

Akizungumzia tukio hilo, Walter Chipeta ambae ni mshirika wa kampuni ya uwakili ya Hallmark Attorneys alisema kufuatia kitendo kilichofanywa na mdeni huyo, kampuni yake imejipanga kuendelea na mkakati wake wa kuhakikisha inafanikiwa kuzipata mali hizo licha ya ukinzania mkubwa kutoka kwa mdeni huyo.

“Hivi hapa tunapoongea tayari tunaendelea na hatua kisheria ambapo pamoja na mambo mengine tayari tumeripoti tukio hilo kwa jeshi la Polisi kwa kuwa mdeni huyu si tu kwamba alituzuia kufanya kazi yetu bali pia alisababisha vurugu ambazo zilitishia usalama wa baadhi ya maofisa wetu” Alisema Bw Chipeta.

Hata hivyo, alipotafutwa kwa njia ya simu, Owais Pardesi ambae ndio Mwenyekiti na mmiliki wa kampuni ya Cosmos Properties hakupatikana kwa njia ya simu na huku pia jitihada za  kumtafuta zikiendelea.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC, SILABU waungana kufikisha elimu ya fedha majumbani

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeingia makubaliano ya ushirikiano...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Serikali kuwakopesha wajasiriamali 18.5bn/- kupitia NMB

Spread the loveSerikali imetenga kiasi cha Sh 18.5 bilioni kwa ajili ya...

Biashara

Cheza kwa kuanzia Sh 400 kushinda mgao wa Expanse Tournament kasino 

Spread the love  UKISIKIA bosi kacheka ujue Maokoto yanafuatia, Kupitia promosheni pendwa...

BiasharaHabari za Siasa

Bunge laitaka Serikali kudhibiti ufisadi miradi ya mkakati

Spread the loveKAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, imeitaka Serikali kuimarisha...

error: Content is protected !!