May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wawili wafariki dunia, 8 wajeruhiwa ajali Kimara-Suka

Spread the love

 

WATU wawili wamefariki dunia na wengine nane kujeruhiwa vibaya baada ya lori aina ya Scania kugonga watu waliokuwa wanavuka barabara ya Morogoro katika eneo la Kimara – Suka jijini Dar es Salaam leo Januari 28, 2022. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea),

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Muliro Jumanne Muliro amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kuongeza kuwa majeruhi hao wamekimbizwa katika hospitali ya Bochi iliyopo eneo la Kwa Msuguru Mbezi jijini humo.

Akifafanua kuhusu ajali hiyo iliyotokea muda wa saa 12:15 asubuhi, Muliro amesema lori hiyo lenye namba za usajili T 814 DGA, likitokea Mbezi kuekelea Ubungo, liliwavamia watu hao waliokuwa wanavuka barabara kwenye kivuko cha waenda kwa miguu maarufu kama ‘Zebra’.

Amesema mmoja wa watu hao wawili waliopoteza maisha, ni mwanafunzi.

Aidha, baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo wamesema lori hilo lililokuwa na tela lilipoteza mwelekeo baada ya kufeli breki.

error: Content is protected !!