Tuesday , 7 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Dart kutumia mfumo mpya ‘mwendokasi,’ mikakati yatangazwa
Habari Mchanganyiko

Dart kutumia mfumo mpya ‘mwendokasi,’ mikakati yatangazwa

Spread the love

 

WAKALA wa Mabasi Yaendayo Haraka (Dart) nchini Tanzania imeanzisha kutumia mfumo mpya wa ukataji wa tiketi wa kielektroniki ili kuhakikisha inazuia upotevu wa mapato. Anaripoti Ibrahim Yamola, Dar es Salaam … (endelea).

Hayo yamesemwa na Meneja wa Teknolokia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) wa Dart, Ng’wanashigi Gagaga leo Ijumaa, tarehe 21 Januari 2022, jijini Dar es Salaam wakati wa semina kuhusu maendeleo ya mradi wa wakala hao kwa wahariri wa vyombo vya habari.

Gagaga amesema, mfumo uliokuwapo haukuwa vizuri na Serikali kuamua kuuondoa na kuanzisha mfumo wake mwenyewe “ambao hautakuwa na gharama kubwa kwani ukiwa na gharama kubwa anayekuja kuumia ni mwananchi.”

“Mfumo wa kutaka tiketi umeanza kufanya kazi kwa tiketi hizi za utambuzi wa QR Code na unafanya kazi ambapo kati ya vituo 33 vituo 20 tayari vimeanza kutumia huu mfumo. Lakini unaweza kutumia kupitia simu za mkonini na au kununua kadi maalum,” amesema Gagaga

Ingawa kwenye mamelezo yake, meneja huyo hakuutaja kwa jina mfumo uliokuwapo, lakini waliokuwa wakitoa huduma eneo la tiketi za kielektroniki ilikuwa Kampuni ya Maxmalipo iliyoacha zaidi ya miaka ya miaka miwili.

Meneja huyo amesema, wanakusudia kufunga mfumo maalum wenye uwezo wa kuangalia mabasi yapishane kwa muda gani “na katikati ya mwaka huu, tunaweza kuwa tumekamilisha kwani hatuutengenezi sisi bali tunaununua na tuko hatua za mwisho za manunuzi.”

Naye Kaimu Mkurgenzi wa Uendeshaji na Usimamizi wa Miundombinu wa Dart, Mhandisi Ahmed Wamala amesema, mradi umegawanyika katika awamu sita ambapo awamu ya kwanza yenye kilomita 20.9 imekwisha kujengwa na kutumika kutoka Kivukoni kwenda Kimara na kutoka Magomeni kwenda Moroco na Fire kwenda Kariakoo.

Wamala amesema, awamu ya pili kutoka katikati ya Jiji kwenda Mbagala Rangi tatu na kutoka JKT Mugulani kuja kukutana na Magomeni, “ujenzi wake unaendelea ambao ulikwekwa mafungu mawili.”

Ametaja mafungu hayo ni ya ujenzi wa miundombinu ya barabara ambapo mkandarasi amefikia asilimia 45 na pili ni miundombinu ya majengo ikiwemo depo umekamilika kwa asilimia 100.

Wamala ametaja awamu ya tatu itahususisha barabara za kutoka mjini kwenda Gongolamboto kupitia Uwanja wa Ndege, “usanifu umekwisha kamilika, tumefanya mchakato wa kumpata mjenzi na tumepata kibali kutoka Benki ya Dunia kumwajili mkandarasi na wakati wowote tutaanza ujenzi.

Awamu ya nne ameitaja ni barabara ya Ali Hassan Mwinyi kuanzia Maktaba kwenda Tegeta hadi Dawasa eneo la Boko na kwenda Ubungo katika daraja la Kijazi. Usanifu umekwisha kufanyika na mtaalamu elekezi amekwisha kuleta nayaraka na kuzipitia na kabla yam waka huu kuisha ujenzi utakuwa umekwenda.

Wamala ametaja awamu ya tano zinahusisha barabara za Mandela pale Ubungo kwenye daraja la Kijazi kwenda Kigamboni katika daraja la Nyerere “halafu tuna barabara mpya tunaitengeneza kutoka Tabata Segerea inakwenda mpaka ‘round about’ ya Kigogo, tayari usanifu umefanyika na serikali inaendelea kufanya majadiliano na wafadhili na kama majadiliano yatakwenda vizuri, Aprili 2022 tunaweza kuwa tumefanya mkataba.”

Awamu ya sita inahusisha barabara ya Mwai Kibaki kutoka Moroco inakwenda kuungana na barabara ya Ali Hassan pale Lugalo.

“Lakini tutakuwa na upanuzi wa barabara kutoka Kimara kwenda Kibaha kwa kuweka njia na vituo maalum na tutakuwa na upanuzi wa Mbagala Rangi tatu kwenda vikindu na tukikamilisha yote haya tutakuwa na kilomita 154.4,” amesema Wamala

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Usafirishaji wa Dar), Mhandisi Fanuel Kalugendo amesema, ili kubaini mabasi mabovu wanashirikiana na Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) ili kuwa inayafanyia ukaguzi na kutoa ushauri ili kuhakikisha wanakuwa na mabasi bora kwa matumizi.

Amesema, kwa kawaida asilimia 90 ya mabasi yawe barabarani na asilimia 10 yanakuwa matengenezo na kwa kipindi hiki wana magari 210 na yanayopaswa kuwa barabarani zaidi ya 190, “lakini ifahamike hatutoi mabasi yote kwenda barabarani kwani mengine lazima yaende matengenezo.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mahakama yatoa uamuzi zuio dhidi ya Club House

Spread the loveMAHAKAMA Kuu ya Tanzania, Masjala Kuu jijini Dar es Salaam,...

Habari Mchanganyiko

GGML, OSHA yawanoa bodaboda 200 Arusha

Spread the loveZAIDI ya madereva bodaboda 200 wa jiji la Arusha wamepatiwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Serikali kuwakopesha wajasiriamali 18.5bn/- kupitia NMB

Spread the loveSerikali imetenga kiasi cha Sh 18.5 bilioni kwa ajili ya...

AfyaHabari Mchanganyiko

Huduma za kibingwa zazinduliwa katika hospitali za halmashauri 184

Spread the loveSERIKALI imezindua huduma za matibabu za kibingwa katika hospitali 184...

error: Content is protected !!