Thursday , 2 May 2024
Home Gazeti Habari Adaiwa kujifanya polisi kwa miaka saba
HabariTangulizi

Adaiwa kujifanya polisi kwa miaka saba

Spread the love

 

MKAZI wa Nyamanoro, Mkoa wa Tabora nchini Tanzania, Abdul Nassoro (49) amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya mkoani humo kwa tuhuma za kujifanya ofisa wa Jeshi la Polisi kwa zaidi ya miaka saba. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Akimsomea jana Jumatatu tarehe 17 Januari 2022, mashitaka yanayomkabili mbele ya Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Juhudi Mdonya, Mwendesha Mashitaka wa Polisi, Elimajid Kweyamba, alisema mshitakiwa anakabiliwa na mashitaka mwili.

Katika shitaka la kwanza la kukutwa na vitambulisho mbalimbali vya kazi, Kweyamba alidai tarehe 24 Desemba 2021 saa 7:45 mchana, maeneo ya Kituo cha Polisi cha Kata ya Igunga Mjini, Nassoro alikamatwa na vitambulisho hivyo, huku kwa zaidi ya miaka saba akijitambulisha kuwa mwajiriwa wa Polisi Tanzania mwenye namba G.3659 Koplo Marko.

Kwa mujibu wa Kweyamba mshitakiwa huyo alitenda kosa hilo kinyume na kifungu 100(b) cha kanuni ya adhabu sura ya 16 mapitio ya 2016.

Katika shitaka la pili ya wizi wa kuaminika, ilidaiwa tarehe 8 Desemba 2021 saa tisa alasiri katika mtaa wa Benki Mpya, kata ya Igunga Mjini Nassoro aliiba Sh milioni 15 alizoaminiwa na kupewa na Kazawadi Bethulabusha ili kumnunulia kilo 32,000 za mchele, lakini hakufanya hivyo wala kurudisha fedha.

Kweyamba alidai pia kwamba mshitakiwa alitenda kosa hilo kinyume na kifungu 273(b) na 265 cha kanuni ya adhabu sura ya 16 mapitio ya 2019.

Hata hivyo, mshitakiwa hakutakiwa kujibu chochote kwa kuwa Mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza shauri hilo na alipelekwa mahabusu baada ya kukosa mdhamini mmoja kwa dhamana ya maandishi ya Sh milioni tatu hadi tarehe 28 Januari 2022 kesi hiyo itakapotajwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Serikali yaanza msako wanaotoa mikopo kausha damu

Spread the loveSERIKALI imeanza kufuatilia watu, vikundi na taasisi zinazotoa kinyume cha...

Habari MchanganyikoTangulizi

Walimu 5000 Songwe waililia CWT kuwanyima sare

Spread the loveZaidi ya walimu 5000 ambao ni wanachama wa Chama cha...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu amjibu Fatma Karume kuhusu Rais Samia

Spread the love  MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Slaa: Watanzania iungeni mkono Chadema uchaguzi 2025

Spread the loveMWANASIASA mkongwe nchini Tanzania, Dk. Wilbroad Slaa, amewataka watanzania wakiunge...

error: Content is protected !!