Saturday , 27 April 2024
Home Gazeti Habari Mrithi wa Ndugai: CCM kufyeka wagombea 67
HabariTangulizi

Mrithi wa Ndugai: CCM kufyeka wagombea 67

Aliyekuwa Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai
Spread the love

 

KAMATI Kuu ya chama tawala nchini Tanzania- Chama Cha Mapinduzi (CCM), kitakuwa na jukumu zito la kufyeka wagombea 67 kati ya 70 walijitosa kumrithi Job Ndugai kuwa spika ili kuwapata watatu watakaokwenda hatua inayofuata. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Itakuwa chini ya mwenyekiti wake, Rais Samia Suluhu Hassan, ambayo inakutaka kuanzia leo Jumanne tarehe 18 Januari 2022 hadi kesho inayochuja na kufanya uteuzi wa mwisho kati ya wagombea wote 70.

Wagombea wote hao, wanawahia kuvaa joho la uspika wa Bunge la Tanzania, baada ya Job Ndugai kujiuzulu nafasi hiyo tarehe 6 Januari 2022

Alichukua uamuzi huo, baada ya kauli yake aliyoitoa kuhusu serikali kuendelea kukopa fedha nje kuibua mjadala mkali ndani ya chama chake na kushinikizwa kujiuzulu.

Kamati hiyo, inakutana ikiwa ni siku moja imepita tangu sekretarieti ya chama hiyo, chini ya uenyekiti wa Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo kujadili wagombea na kuishauri kamati kuu hiyo.

Ratiba iliyotolewa na CCM ya mchakato mzima, mara baada ya kamati kuu kukamilisha kazi yake, itateua wagombea watatu ambao hao watakwenda kupigiwa kura na kamati ya wabunge wote wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Vigogo wa Bunge, mawaziri wastaafu, wanasheria, wasomi na wanachama wa kawaida wamejitosa kwenye mbio hizo ambao wote 70 wanapitishwa katika chujio la kumpata mmoja atakayekwenda kushindanishwa na wa vyama vingine.

Kati ya waliojitoza kwenye mbio hizo, wamo vigogo wa sasa wa Bunge kama Naibu Spika, Dk. Tulia Ackson, Mwenyekiti waBunge, Mussa Zungu na waliowahi kuongoza Bunge kwa maana ya mwenyekiti, Andrew Chenge ambaye amewahi kuwa mwanasheria mkuu wa serikali watachuana kwenye kinyang’anyiro hicho.

Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashililah naye ni miongoni mwa waliochukua fomu akitaka kurejea kwenye uongozi wa muhimi huo pamoja na Asia Abdallah, Angelina John na waziri wa zamani katika serikali ya awamu ya nne aliyehudumu pia nafasi ya mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa chama hicho Taifa (UWT), Sophia Simba.

Aidha, wamo wabunge, Joseph Msukuma wa Geita Vijijini, Godwin Kunambi wa Mulimba mkoani Morogoro, Luhaga Mpina wa Kiseka mkoani mwanza pamoja na Emmanuel Mwakasaka waTabora Mjini ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge.

Kuna mawaziri wa zamani wa mifugo na uvuvi, Dk. Titus Kamani ambaye mwaka 2015 alikuwa kati ya wanachama 38 wa CCM waliochukua na kurejesha fomu ya kuwania urais ndani ya chama hicho lakini hakufanikiwa.

Aliyewahi kuwa naibu waziri wa nishati na madini wakati wa utawala wa awamu ya nne wa Jakaya Kikwete akiwakilisha wananchi wa Shinyanga Mjini, Stephen Masele naye amechukua fomu.

Masele amewahi kuwa Makamu wa Kwanza waRais wa Bunge la Afrika (PAP).

Katika hao 69, kuna msomi mwenye shahada mbalimbali tisa kutoka vyuo vya ndani na nje ya Tanzania, Profesa Handley Mafwenga.

Wengine kwenye kinyang’anyiro hicho ni, Dk. Saimon Ngatunga, Tumsifu Mwansamale, Merkion Ndofu, Ambwene Kajula, Patrick Nkandi, Hamidu Chamani na Goodluck Ole-Madeve.

Pia, wamo Juma Chum, Baraka Byabato, Dk Musa Ngonyani, Faraji Rushagama, Hamisi Rajabu, Festo Kipate, George Nangale, Barua Mwakilanga, Zahoro Hanuna na Thomas Kirumbuyo na Mhandisi AbdulAziz Jaad Hussein.

Mbio hizo zimewashuhudia wengine wakijitosa kama Hatibu Mgeja, Dk. Linda Ole Saitabau na Mbunge wa zamani wa Makete, Profesa Norman Sigalla King, Emmanuel Sendama, Bibie Mssumi, Hilal Seif, Athumani Mfitakamba, Mwenda Mwenda na Mbunge wa zamani wa Ulanga, Goodluck Mlinga.

Wengine ni, Herry Kessy, Josephat Malima, Adam Mnyavanu, Andrew Kevela na Mbunge wa Nyasa, Stella Manyanya.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

Habari za SiasaTangulizi

Shibuda amlima waraka mzito Bulembo

Spread the loveMKONGWE wa siasa nchini, John Shibuda amemshukia kada maarufu wa...

error: Content is protected !!