Tuesday , 7 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Kesi ya Mbowe: Shahidi aliyeugua ghafla kizimbani, anatoa ushahidi
Habari Mchanganyiko

Kesi ya Mbowe: Shahidi aliyeugua ghafla kizimbani, anatoa ushahidi

Spread the love

 

SHAHIDI wa kumi wa Januari, Innocent Ndowo (37) katika kesi ya ugaidi inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe na wenzake watatu, anaendelea kutoa ushahidi wake, mbele ya Jaji Joachim Tiganga. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Ndowo ambaye ni askari polisi aliyebobea katika uchunguzi wa kisayansi anayeweza kuingia mawasiliano ya simu, jana Jumatatu, tarehe 17 Januari 2022, aliugua ghafla kichwa akiwa kizimbani, wakati anaendelea na ushahidi wake.

Kutokana na hatua hiyo, Jaji Tiganga aliamua kuiahirisha hadi leo Jumanne, kuangalia kama Ndowo aliyepata mafunzo ndani na nje ya Tanzania wa eneo hilo la uchunguzi atakuwa ameimalika.

Mbali na Mbowe kwenye kesi hiyo, wengine katika kesi hiyo yenye mashtaka sita ya ugaidi, ni waliokuwa makomandoo wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Halfan Bwire Hassan, Adam Kasekwa na Mohammed Abdillah Ling’wenya.

Alidai vielelezo hivyo alivipokea tarehe 13 Agosti 2020, kutoka Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), na kwamba alipangwa kuvifanyia uchunguzi katika maeneo matatu, ambayo ni mawasiliano kupitia mitandao ya kijamii ya Telegram, WhatsApp, Facebook na ujumbe mfupi wa maneno.

Eneo la pili ni taarifa za usajili na miamala ya fedha na la mwisho ikiwa ni la mawasiliano ya kupiga na kupigwa za namba za simu zilizokutwa katika simu hizo nane.

Alidai uchunguzi wake ulibaini simu nne kati ya nane zilikuwa na shahidi na nne zilizobakia hazikuwa na ushahidi.

Alidai, baada ya kumaliza uchunguzi huo, alikabidhi ripoti za uchunguzi, kwa Askari Polisi aliyemtaja kwa jina la Inspekta Swilla.

Endelea kufuatilia MwanaHALISI Online, MwanaHALISI TV kwa habari na taarifa mbalimbali

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mahakama yatoa uamuzi zuio dhidi ya Club House

Spread the loveMAHAKAMA Kuu ya Tanzania, Masjala Kuu jijini Dar es Salaam,...

Habari Mchanganyiko

GGML, OSHA yawanoa bodaboda 200 Arusha

Spread the loveZAIDI ya madereva bodaboda 200 wa jiji la Arusha wamepatiwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Serikali kuwakopesha wajasiriamali 18.5bn/- kupitia NMB

Spread the loveSerikali imetenga kiasi cha Sh 18.5 bilioni kwa ajili ya...

AfyaHabari Mchanganyiko

Huduma za kibingwa zazinduliwa katika hospitali za halmashauri 184

Spread the loveSERIKALI imezindua huduma za matibabu za kibingwa katika hospitali 184...

error: Content is protected !!