May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Simba wapoteza mchezo wa kwanza dhidi ya Mbeya City

Spread the love

 

KLABU ya soka ya Simba imepoteza mchezo wake wa kwanza kwenye Ligi Kuu Tanzania mara baada ya kukubali kichapo cha bao 1-0, dhidi ya Mbeya City. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Mchezo huo wa mzunguko wa kwanza ulipigwa hii leo tarehe 17 Januari 2022 kwenye dimba la Sokoine Jijini Mbeya ambapo Mbeya City walikuwa wenyeji wa mchezo huo.

Kabla ya mchezo huo Simba ilicheza michezo  10 bila kupoteza kwenye Ligi Kuu, lakini rekodi hiyo ilifunjwa hii leo kwa baoa la dakika ya 19 lililowekwa kambani na Paul Nonga mshambuliaji mkongwe wa timu hiyo.

Kwenye mchezo huo Simba ilikuwa na uwezekano wa kuchomoa bao hilo, mara baada ya kukopata penati kwenye dakika ya 47, lakini walishindwa kuitumia nafasi hiyo kufuatia Chriss Mugalu kukosa pigo hilo la penati mara baada ya mpira kugonga nguzo ya goli.

Mchezo huo uligubikwa na matukio mengi likiwepo la kuoneshwa kadi nyekundu kwa mlinzi wa Mbeya City Mpoki Mwakinyuke Kwenye dakika ya 43 kufuatia kumchezea vibaya mshambuliaji wa klabu ya Simba Chriss Mugalu na kufanya timu hiyo kumaliza mchezo huo wakiwa pungufu.

Mara baada ya kupoteza mchezo huo Simba inaendelea kusalia kwenye nafasi ya pili wakiwa na pointi 24 Nyuma ya Yanga ambao ni vinara wa Ligi hiyo kwenye msimamo wakiwa na pointi 32.

Kufuatia kuacha alama tatu mkoani Mbeya kikosi hiko kitafunga safari mpka mkoani Morogoro ambapo siku ya Jumamosi Januari 22, mwaka huu kitashuka dimbani kwenye dimba la Jamhuri kuwakabili Mtibwa Sugar ambao mchezo wa mwishoa walienda sare ya bao 1-1.

Kwa upande wa Mbeya City alama hizo tatu dhidi ya Simba zimewapandika mpaka kwenye nafasi ya tatu kwenye msimamo wakiwa na pointi 19 na kuwashsha timu ya Polisi Tanzania katika nafasi hiyo waliyokaa kwa muda mrefu.

error: Content is protected !!