May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Samia ateua viongozi 2

Spread the love

 

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi wawili akiwemo Mcha Hassan Mcha kuwa Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA). Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Kabla ya uteuzi huo, Mcha alikuwa Kamishna wa Udhibiti na Utekelezaji, Makao Makuu ya TRA ambaye anachukua nafasi ya Msafiri Mbibo ambaye ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Madini.

Uteuzi huu wa Mcha umeanza tarehe 5 Desemba 2021.

Aidha, Rais Samia amemteua Balozi Celestine Mushy kuwa Balozi wa Tanzania nchini Austria.

Balozi Mushy alikuwa Katibu Tawala Msaidizi, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara ambaye uteuzi wake umeanza tarehe 14 Januari 2022.

Taarifa hii ya uteuzi, imetolewa leo Jumanne, tarehe 18 Januari 2022 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Jaffar Haniu.

error: Content is protected !!