Sunday , 5 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa ACT-Wazalendo yawaonya wanaotaka kukiendesha, kukiburuza
Habari za Siasa

ACT-Wazalendo yawaonya wanaotaka kukiendesha, kukiburuza

Ado Shaibu, Katibu Mkuu ACT-Wazalendo
Spread the love

 

KATIBU Mkuu wa Chama cha ACT- Wazalendo nchini Tanzania, Ado Shaibu, amesema chama chake kinataka kujitofautisha na vyama vingine, hivyo hakitakubali kuendeshwa kwa kuburuzwa na au msukumo kutoka kwa chama kingine. Anaripoti Mwandishi Wetu, Ruvuma … (endelea).

Ado ametoa kauli hiyo jana Jumanne, tarehe 21 Desemba 2021, akielezea hostia ya kuanzishwa kwa ACT-Wazalendo mwaka 2014, wakati akizungumza na wanachama wake wa Wilaya ya Nyasa, mkoani Ruvuma.

“Lazima mfahamu chama hiki hakitoendeshwa kwa matakwa ya chama kingine chochote cha siasa, ACT-Wazalendo hakitoendeshwa wala kuburuzwa na maelekezo, msukumo na ushawishi wa chama kingine chochote cha siasa. Kitaendeshwa kwa misngi ambayo tumejiwekea kwenye katiba,” amesema Ado.

Katibu Mkuu huyo wa ACT-Wazalendo, amesema chama hicho kinataka kujitofautisha na vyama vingine kwa kuwa mfano kwenye siasa za kistaarabu na za kuwakomboa Watanzania masikini kiuchumi.

“Kwa hiyo chama hiki kinataka kujitofautisha na vyama vingine, tunataka kuwa chama bora na cha mfano ambacho kitajipambanua kwa siasa za kistaarabu, za kuwakomboa Watanzania masikini na siasa za masuala ya maslahi ya wakulima, wafanyakazi na wafanyabiashara,” amesema Ado.

Ado amesema, ACT-Wazalendo kilianzishwa baada ya kuona Tanzania inakosa siasa zisizojikita katika kutatua matatizo ya wananchi.

Ado Shaibu, Katibu Mkuu wa ACT-Wazalendo akizungumza na wanachana wa chama hicho katika jimbo la Nyasa mkoani Ruvuma.

“Wakati chama hiki kinaanzishwa mwaka 2014, ni muhimu mfahamu kilizaliwa kutokana na mapungufu. Nchi nzima lazima wafahamu hili, kulikuwa na upungufu wa mfumo wa uendeshaji siasa za nchi yetu, siasa ziligubikwa na ubabaishaji, kukosa uwazi, uadilifu na kukosekana kwa uzalendo,” amesema Ado na kuongeza:

“Siasa ziligubikwa na viongozi ambao wanamsahau mwananchi mnyonge wa vijijini na mjini, viongozi wa vyama tulikuwa hatujajikita katika siasa za kumkomboa mwananchi masikini. Ndiyo zilikuwa siasa za Tanzania.”

Ado yuko katika ziara ya Sekretarieti ya ACT-Wazalendo Taifa, iliyoanza tarehe 20 Desemba mwaka huu, ambapo atatembelea mikoa ya Ruvuma, Mtwara, Lindi, Pwani na Tanga.

Ziara hiyo inalenga kukijenga chama hicho ikiwa pamoja na kuwaandaa wanachama wake kuhusu mabadiliko ya uendeshaji wake kisayansi .

Kauli hiyo ya Ado imekuja siku kadhaa baada ya baadhi ya wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kukosoa hatua ya Kiongozi wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, ya kumuombea radhi mwenyekiti wake, Freeman Mbowe, anayesota rumande miezi mitano, akikabiliwa na mashtaka ya ugaidi.

Zitto alitumia kikao cha wadau wa tasnia ya siasa, kilichoandaliwa na Baraza la Vyama vya Siasa nchini, ambacho Chadema kiligoma kushiriki, kumuomba Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amsamehe Mbowe ili aachwe huru kwa ajili ya kujenga umoja wa kitaifa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Mbatia ambwaga Selasini, mahakama yaamuru alipwe fidia

Spread the loveMAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, imemuamuru...

Habari za SiasaTangulizi

Mkulo afariki dunia, kuzikwa kesho Kilosa

Spread the loveALIYEKUWA Waziri wa Fedha na Mbunge wa Kilosa (CCM), Mustafa...

Habari za SiasaTangulizi

Sabaya afutiwa kesi, ruksa kugombea uongozi

Spread the loveMwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali DPP leo Ijumaa amefuta rufaa...

Habari za Siasa

Serikali yasaka bilioni 3 kujenga daraja Mto Mpiji

Spread the loveSerikali imesema inaendelea na juhudi za kutafuta fedha kiasi cha...

error: Content is protected !!