Sunday , 29 January 2023
Home Kitengo Maisha Afya Mpango wa pili chanjo Korona wazinduliwa, laki moja kuchanjwa kila siku
Afya

Mpango wa pili chanjo Korona wazinduliwa, laki moja kuchanjwa kila siku

Spread the love

 

SERIKALI ya Tanzania, inatarajia kuchanja chanjo ya Ugonjwa wa Virusi vya Korona (UVIKO-19), kwa wananchi 80,000 hadi 100,000 kwa siku, kupitia mpango wake wa harakishi na shirikishi kwa jamii awamu ya pili, dhidi ya janga hilo. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Taarifa hiyo imetolewa leo Jumatano, tarehe 22 Desemba 2021 na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Profesa Abel Makubi, katika uzinduzi huo uliofanywa na Waziri wa Afya, Dk. Dorothy Gwajima, jijini Arusha.

“Katika huu mpango tuna lengo la kufikia kuchanja wananchi 80,000 mpaka 100,000 kwa siku. Huu mpango unatuondoa kwenye kuchanja watu 20,000, 30,000 na 40,000, unatupeleka kwenda kuchanja watu 80,000 hadi 100,000 kwa siku moja,” amesema Prof. Abel Makubi.

Katibu mkuu huyo wa Wizara ya afya, amesema kila mkoa utatakiwa kuchanja wananchi kuanzia 4,000 hadi 5,000 kwa siku, ili baada ya miaka miwili asilimia 60 ya watu wawe wamepata kinga hiyo dhidi ya UVIKO-19.

Prof. Makubi amesema, ili lengo hilo liweze fanikiwa, Serikali imeongeza vituo vya utoaji chanjo.

“Tunaongeza vituo kutoka 6,784 viwe zaidi ya 7,000 hadi 8,000. Pamoja na kuweka sehemu z a kuchanja kwenye mitaa, hawa wahudumu katika ngazi ya jamii watakuwa kwenye mitaa mbalimbali kuweka mahema, vituo na hata kwenye nyumba hadi nyumba, kuelimisha wananchi waweze kuchanja,” amesema Prof. Makubi.

Prof. Makubi amesema, hadi kufikia tarehe 18 Desemba 2021, Serikali imepokea dozi milioni 4.4 za chanjo ya UVIKO-19, ikiwemo aina ya Pfizer na Sinopharm .

1 Comment

  • Haitoshi hata kidogo. Tuwe serious. Maambukizi yameshika kasi. Mgonjwa mmoja aliyeambukizwa POSITIVE ameenda hospitali akapewa vidonge na kurudishwa nyumbani bila ya barakoa wala chanjo ili azidi kuwaambukiza wana familia na jamii kwa ujumla.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Afya

JK atoa ya moyoni kuhusu huduma za afya

Spread the love  RAIS Mstaafu Dk. Jakaya Kikwete amesema huduma za afya...

AfyaHabari za Siasa

Heche amvaa Ummy Mwalimu kisa bima ya afya

Spread the love  MJUMBE wa Kamati Kuu ya Chadema, John Heche amemtaka...

Afya

Asilimia 86 wenye umri zaidi ya miaka 18 wapata dozi kamili ya Uviko-19

Spread the love  KWA kipindi cha miezi sita kuanzia mwezi Julai hadi...

Afya

Waziri anusa ufisadi matumizi fedha za UVIKO-19

Spread the love  NAIBU Waziri wa Afya, Dk. Godwin Mollel, ameagiza uchunguzi...

error: Content is protected !!