Monday , 6 May 2024
Michezo

Spread the love

Simba waigomea TFF

KATIKA hali ya kushangaza uongozi wa klabu ya Simba ulimzuia kocha wake mkuu Pablo Franco Martin kutoongea na waandishi wa Habari, kufuatia uwepo wa bango lenye lenye nembo ya kampuni ya Gsm ambao ni sehemu ya udhamini wa Ligi hiyo kufuatia klabu hiyo kutotambua mkataba huo. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Mkutano huo dhidi ya waandishi wa habari ambao huko kikanuni ambao unatakiwa kufanyika siku moja kabla ya mchezo kwa makocha wa timu zote mbili kuzungumzia maandalizi kuelekea mchezo husika.

Kwenye mkutano huo ambao ulifanyika leo Disemba 10, mwaka huu majira ya saa 6 mchana kwenye ukumbi wa mikutano wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF, uliopo Ilala, Dar es Salaam uliudhuliwa na kocha wa Yanga tu, Mohammed Nasreddine Nabi.

Kocha huyo wa klabu ya Simba alifika mchana akiambatana na maafisa wa klabu hiyo kitengo cha Habari na mawasiliano na mara baada ya Nabi kumaliza kuongea na waandishi wa Habari, maafisa hao waliingia kwenye ukumbi huo na kutanga bango hilo lenye nembo ya Gsm kutolewa, lakini jambo hilo halikufananikiwa na wakaamua kumuondoa kocha wao kwenye viunga hivyo.

Sintofahamu hii inatokea ikiwa siku chache toka klabu ya Simba ilipoandika barua kwenda Bodi ya Ligi ya kutaka ufafanuzi wa mkataba ambao Tff uliingia dhidi ya kampuni ya Gsm ya udhamini mwenza wa Ligi Kuu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Ligi mbalimbali za pesa kuendelea leo

Spread the love JUMAPILI ya leo imekaa kipesa tuu yani baada ya...

Michezo

Usiishie kuangalia tu game za leo, piga na mkwanja na Meridianbet

Spread the love  LIGI mbalimbali barani ulaya zitarejea tena Jumamosi ya leo...

Michezo

Ligi mbalimbali za pesa kuendelea leo

Spread the love Ijumaa ya leo ambapo mechi mbalimbali zinaendelea Duniani Meridianbet...

Michezo

Europa na Conference kukupatia pesa ndefu leo

Spread the love  ALHAMISI ya leo tutaenda kushuhudia mitanange ya kukata na...

error: Content is protected !!