January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Guardiola, Trend watamba tuzo mwezi Novemba Epl

Pep Guardiolla

Spread the love

 

Kocha wa klabu ya Manchester City Pep Guardiola amechaguliwa kuwa kocha bora wa mwezi Novemba kwenye Ligi Kuu nchini England “EPL”,. Huku beki wa kulia wa klabu ya LiverPool Trend Alexander Arnold akichagulia kama mchezaji bowa wa Ligi hiyo kwa mwezi Novemba. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Ndani ya mwezi Novemba Beki huyo wa kulia wa Liverpool amecheza michezo mitatu, huku akifunga bao moja na kutoa pasi za mabao (assist) nne, katika mabao 10 yaliyofungwa na timu hiyo katika michezo hiyo mitatu.

Katika kinyang’anyiro hiko mchezaji huyo alikuwa akichuanao na Joao Cancelo na Bernardo Silva wote kutoka Manchester City, Diogo Jota kutoka Liverpool, Emmanuel Dennis Watford, na John McGinn wa Aston Villa.

Kwa upande wa Guardiola, katika mwezi Novemba amefanikiwa kuiongoza Manchester City kwenye michezo mitatu na kushinda yote na hivyo kutwaa tuzo hii kwa mara ya 10 toka alipojiunga na klabu hiyo.

error: Content is protected !!