January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Polepole awaanika ‘wahuni’ 

Humphrey Polepole

Spread the love

 

ALIYEKUWA Katibu wa NEC- Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), amesema watu aliowataja kuwa wahuni ambao hawajashughulikiwa, ni wale wanaohangaika na masilahi yao binafsi badala ya Taifa. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Polepole ametoa kauli hiyo leo Jumamosi, tarehe 11 Desemba 2021, akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam.

Mbunge huyo wa kuteuliwa na Rais, alitoa ufafanuzi huo baada ya kuibuka mjadala mitandao, kufuatia kauli yake  iliyodai kuwa, alitamani Serikali ya Awamu ya Tano, chini ya Hayati John Magufuli, ingemaliza watu aliowaita wahuni.

Polepole amewajibu watu waliotaka orodha ya  wahuni  ambao hawajashughulikiwa, waende katika Mamkala ya Mapato Tanzania (TRA) na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (Takukuru), watapa orodha hiyo.

“Wahuni watapenda maslahi binafsi na wapo,  Nikasema wahauni wakwepa kodi wapo TRA watakueleza, wabadhirifu wa mali ya umma wapo, nenda Takukuru wapo wengine wanaendelea kuhojiwa. Nasema wahuni wanaibuka watu, wanasema niambie hivi na sisi ni wahuni? Nawatazama,” amesema Polepole.

Polepole amesema kuwa, hatoacha kuwaanika watu aliowaita kuwa wazinguaji.

“Kuna majitu mengine ni viongozi wanachekelea kuitwa wahuni, nikasema ipo kazi. Nazungumza hivi  katika hatua ya mwanzo,  watu wakizingua pahala natoka tena nasema hapo wanazingua,” amesema Polepole.

Miongoni mwa watu waliotaka kujua orodha ya wahuni hao, ni Mbunge wa Mtama, mkoani Lindi (CCM), Nape Nnauye, kupitia ukurasa wake wa Twitter aliandika akisema anatamani kujua wahuni waliopona.

error: Content is protected !!