Friday , 3 May 2024
Home Kitengo Michezo Yanga yaendelea kukusanya pointi, yaipiga KMC
Michezo

Yanga yaendelea kukusanya pointi, yaipiga KMC

Spread the love

 

TIMU ya Yanga ya jijini Dar es Salaam, imeendelea kuonesha makucha yake katika ligi kuu NBC Tanzania Bara 2021/22, kwa kujikusanyia pointi tatu muhimu. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea).

Ni baada ya kuutumia vyema Uwanja wa Majimaji, Songea mkoani Ruvuma leo Jumanne, tarehe 19 Oktoba 2021, kwa kuwafunga KMC FC ya Kinondoni 2-0.

Vijana hao wa Jangwani, walitumia dakika 11 za kipindi cha kwanza kujihakikishia ushindi.

Alikuwa ni Fiston Mayele dakika ya nne aliyeanza kupeleka shangwe kwa vijana hao wa Jangwani kwa kuunganisha pasi ya mwisho iliyochezwa na kiungo mahiri kwa sasa, Feisal Salum maarufu ‘Fei Toto.’

Yanga wakicheza kandanda safi na la kuvutia kwa kuliandama lango la vijana wa Kinondoni KMC, iliwachukua dakika saba baadaye yaani dakika ya 11, kwa Fei Toto kupiga shuti kali nje ya 18 na kwenda moja kwa moja langoni na kumwacha mlinda mlango Farouk Shikalo asijue la kufanya.

Kwa ushindi huo, Yanga imefikisha pointi tisa, baada ya kushinda mechi zote tatu alichoza. Alianza kwa ushindi wa 1-0 dhidi ya Kagera Sugar na Geit Gold Mine ambayo nayo alishinda 1-0.

Baada ya kutoka Songea kwenye mchezo huo ambao KMC wameutimia uwanja wa Majimaji kama wa nyumbani, Yanga watatua tena dimbani, tarehe 30 Oktoba 2021, kucheza na vijana wa Chamanzi, Azam FC.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Europa na Conference kukupatia pesa ndefu leo

Spread the love  ALHAMISI ya leo tutaenda kushuhudia mitanange ya kukata na...

Habari MchanganyikoMichezo

Wanamichezo Mei Mosi wachangia wahitaji vitu vya mil. 11.5

Spread the loveWanamichezo wanaoshiriki Michezo ya Mei Mosi Taifa 2024 jijini Arusha...

Michezo

Usiku wa Ulaya umerejea kibabe kabisa

Spread the love  LIGI ya Mabingwa barani Ulaya imerejea tena na awamu...

Habari MchanganyikoMichezo

Mambo ya Ndani, Ulinzi zang’ara michezo ya Mei Mosi Arusha

Spread the loveRais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini (TUCTA), Tumaini...

error: Content is protected !!