December 1, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Askofu Mwamakula aendesha maombi mahakamani kesi ya Mbowe

Spread the love

 

ASKOFU wa Kanisa la Uamsho la Moravian, Emmaus Mwamakula, ameendesha maombi maalum katika Mahakama Kuu, Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi kabla kesi inayomkabili kiongozi wa chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania cha Chadema, Freeman Mbowe na wenzake kuanza. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Askofu Mwamakula ameendesha maombi hayo leo Jumatano, tarehe 20 Oktoba 2021, kabla ya mahakama hiyo haijaanza kutoa uamuzi dhidi ya kesi ndogo ndani ya kesi kubwa ya kupinga maelezo ya onyo ya mshtakiwa wa pili katika kesi ya msingi ya uhujumu uchumi, Adam Kasekwa, yasitumike mahakamani hapo kama sehemu ya ushahidi wa jamhuri.

Akiwaongoza mawakili wa utetezi, Askofu Mwamakula amemuomba Mungu aingilie kati kesi hiyo, ili haki itendeke. Wakati wa maombi hayo, mawakili hoa na watu wengine walisimama wakati maombi yakiendelea.

Mahakama hiyo mbele ya Jaji Kiongozi Mustapha Siyani, ilipanga kutoa uamuzi wa kesi hiyo ndogo jana tarehe 19 Oktoba 2021, lakini ilishindikana kutokana na kuwa siku kuu ya maulid, hivyo imepanga kutoa leo.

Kesi hiyo ndogo ndani ya kesi ya msingi, imetokana na mapingamizi ya upande wa utetezi, dhidi ya maelezo ya onyo ya mshtakiwa wa pili, Kasekwa, yaliyowasilishwa mahakamani hapo na upande wa jamhuri kama sehemu ya ushahidi wake.

Wakitaka yasitumike kwa madai kuwa yalichukuliwa kinyume cha sheria, ikiwemo mtuhumiwa kuchukuliwa maelezo hayo nje ya muda, bila ya ridhaa yake.

Mbali na Mbowe na Kasekwa, watuhumiwa wengine katika kesi ya msingi ya uhujumi uchumi yenye mashtaka ya kula njama za kufanya vitendo vya ugaidi ni, Halfan Hassan Bwire na Mohammed Abdillah Ling’wenya.

Miongoni mwa mawakili wanaomuwakilisha Mbowe na wenzake katika kesi ya msingi ni, Peter Kibatala, John Mallya, Jeremiah Mtobesya, Fredy Kiwhelu, Dickson Matata, Alex Masaba na Nashon Nkungu.
Wakati wa jamhuri wakiwa ni pamoja na Mawakili wa Serikali Waandamizi, Robert Kidando, Abdallah Chavula, Pius Hilla, Nassoro Katuga, Jenetreza Kitali, Tulumanywa Majigo na Ester Martin.

Endelea kufuatilia MwanaHALISI TV, MwanaHALISI Online na mitandao yetu ya kijamii kujua kinachoendelea mahakamani hapo

error: Content is protected !!