Tuesday , 7 May 2024
Home Kitengo Michezo Mlinzi Yanga apata pigo
Michezo

Mlinzi Yanga apata pigo

Spread the love

 

BEKI wa kulia wa timu ya wananchi- Yanga SC. Paul Godfrey Nyang’anya maarufu kama ‘Boxer’ amepata pigo baada ya kuondokewa na baba yake mzazi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam …  (endelea).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na klabu hiyo yenye maskani yake mitaa ya Jangwani, kifo cha mzazi huyo wa Boxer kimetokea leo jijini Dar es Salaam.

Taarifa hiyo iliyotolewa kwenye akaunti rasmi ya Yanga katika mtandao wa Instagram, imesema; ” Klabu ya Yanga imepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha Baba mzazi wa mchezaji wetu, Paul Godfrey Nyang’anya klilichotokea leo jijini Dar es Salaam.

“Kwa niaba ya wanachama, wapenzi na mashabiki wa Yanga, uongozi wa Yanga unatoa pole kwa mchezaji wetu Paul na familia yake yote kwa msiba huo mzito na kwamba klabu iko pamoja naye katika kipindi hiki cha majonzi. Bwana ametoa na Bwana ametwaa, Jina lake lihimidiwe.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Idris Sultan anogesha msimu wa 3 wa Bridgerton

Spread the loveSTAA wa burudani kutoka ardhi ya Tanzania, Idris Sultan amenogesha...

Michezo

Ligi mbalimbali za pesa kuendelea leo

Spread the love JUMAPILI ya leo imekaa kipesa tuu yani baada ya...

Michezo

Usiishie kuangalia tu game za leo, piga na mkwanja na Meridianbet

Spread the love  LIGI mbalimbali barani ulaya zitarejea tena Jumamosi ya leo...

Michezo

Ligi mbalimbali za pesa kuendelea leo

Spread the love Ijumaa ya leo ambapo mechi mbalimbali zinaendelea Duniani Meridianbet...

error: Content is protected !!