Thursday , 2 May 2024
Home Kitengo Michezo Twiga Stars yafanya kufuru COSAFA, Rais Samia aimwagia sifa
MichezoTangulizi

Twiga Stars yafanya kufuru COSAFA, Rais Samia aimwagia sifa

Spread the love

 

TIMU ya soka ya Wanawake ya Tanzania ‘Twiga Stars’ imenyakua ubingwa wa michuano ya nchi za ukanda wa kusini mwa Afrika (Cosafa) 2021. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea). 

Twiga walioshiriki michuano hiyo kama wageni waalikwa, wamekinyakua kikombe cha ubingwa leo Jumamosi, tarehe 9 Oktoba 2021 nchini Afrika Kusini.

Ni baada ya kuwafunga Malawi bao 1-0, lililowekwa kambani na Enekia Kasonga dakika ya 64.

Katika michuano hiyo, Twiga Stars imecheza michezo mitano ukiwemo wa fainali na kushinda yote mitano.

Aidha, Amina Allya wa Twiga Stars, amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa michuano hiyo huku Janeth Simba wa timu hiyohiyo akinyakua tuzo ya kipa bora.

Nafasi ya kocha bora nayo imekwenda kwa Bakari Shime wa Twigwa Stars.

Mara baada ya Twiga Stars kutwaa ubingwa huo, pongezi zimetolewa na watu mbalimbali kupitia mitandao ya kijamii akiwemo Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.

Kupitia ukurasa wa Twitter, Rais Samia ameandika “Naipongeza timu yetu ya Taifa ya Wanawake (Twiga Stars) kwa kutwaa ubingwa wa Mashindano ya COSAFA Wanawake 2021.”

“Ubingwa huu unatuletea heshima, unaitangaza nchi yetu na kutia chachu kwa vijana wetu kushiriki michezo. Naipongeza TFF na wote walioshiriki kuiandaa timu yetu.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Europa na Conference kukupatia pesa ndefu leo

Spread the love  ALHAMISI ya leo tutaenda kushuhudia mitanange ya kukata na...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali yaanza msako wanaotoa mikopo kausha damu

Spread the loveSERIKALI imeanza kufuatilia watu, vikundi na taasisi zinazotoa kinyume cha...

Habari MchanganyikoTangulizi

Walimu 5000 Songwe waililia CWT kuwanyima sare

Spread the loveZaidi ya walimu 5000 ambao ni wanachama wa Chama cha...

Habari MchanganyikoMichezo

Wanamichezo Mei Mosi wachangia wahitaji vitu vya mil. 11.5

Spread the loveWanamichezo wanaoshiriki Michezo ya Mei Mosi Taifa 2024 jijini Arusha...

error: Content is protected !!