October 18, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Tyson Fury amtwanga Wilder kwa mara ya pili, achota bilioni 23

Spread the love

 

Bondia Tyson Fury kutoka Uingereza leo tarehe 10 Oktoba, 2021 amemtwanga kwa knock out katika raundi ya 11 bondia Deontay Wilder kutoka Marekani katika mpambano wa kuwania mkanda wa ubingwa wa Uzito wa Juu ‘WBC’ kwenye ukumbi wa T-Mobile Las vegas nchini Marekani. Anaripoti Mwandishi wetu.

Mabondia hao wamekutana kwa mara ya tatu ndani ya kipindi cha miaka mitatu huku Fury akiibuka mshindi katika mapambano mawili.

Katika mpambano wa kwanza uliopigwa mwaka 2018, mabondia hao walitoka sare licha ya Fury kulalamika kuwa marefa walimyima pointi.

Mpambo wa pili ulipigwa Februari mwaka jana ambapo Fury ambaye ni bondia namba moja duniani katika uzani wa uzito wa juu alimshinda Wilder kwa TKO yaani mwamuzi alisitisha pambano hilo kuzingatia usalama wa Wilder katika raundi ya saba na kumpa ushindi Fury.

Pambano la leo kati ya Wilder na Fury lilikuwa lichapwe mwaka huu majira ya joto, lakini likaahirishwa kutokana na Fury kupata ugonjwa wa Covid-19, likapangwa kufanyika mwezi huu wa Oktoba.

Baada ya kuahirishwa Fury alirejea nyumbani kwao Uingereza kwa mkewe Paris ambaye alikuwa amejifungua mtoto wake wa sita, Athena ambaye alitumia siku kadhaa kwenye uangalizi maalumu.

Hata hivyo, baada kushinda pambano hilo, Fury amesema “Lilikuwa pambano kubwa, linastahili kuwa filamu bora ya mwaka. Siwezi kubisha kuwa Wilder ni mpiganaji wa hali ya juu, alinipa ushindani na pesa. Huwa nasema mimi ndiye mpiganaji bora duniani na yeye ndiye wa pili kwa ubora,” amesema.

Hapo awali Furry tayari alikuwa anashikilia mataji ya WBA (super), IBF, WBO na IBO kutokana na ushindi wake dhidi ya Wladimir Klitschko Novemba 2015.

Rekodi zinaonesha kuwa kabla ya mpambano wa leo 12:30 asubuhi, Fury tokea aanze masumbwi, amepigana mapambano 31, akishinda mara 30 na kutoa sare mara 1 tena ni mwaka 2018 dhidi ya Wilder ilhali hajawahi kupigwa au kupoteza pambao.

Wakati Deonay Wilder amepigana mapambano 42, ameshinda mara 4, sare 1 na kipigo 1 vyote kutoka kwa Tyson Fury.

Hata hivyo, kwa mujibu wa mtandao wa TotalSportal Fury alikuwa anatarajiwa kubeba dola za Marekani milioni 10 sawa na Sh bilioni 23 ilihali Wilder akitarajiwa kubeba Sh bilioni 18.

Aidha, kwa mujibu wa takwimu za mtandao wa Celebrity Net, mabondi wote wawili wa utajiri wa dola za Marekani bilioni 30 sawa na Sh bilioni 69.1

error: Content is protected !!