Sunday , 28 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Cheki Naibu Rais alivyowakaribisha walinzi wapya… wanywa chai pamoja
Kimataifa

Cheki Naibu Rais alivyowakaribisha walinzi wapya… wanywa chai pamoja

Spread the love

 

NAIBU Rais wa Kenya, William Ruto amefanya mkutano na maofisa wapya wa ulinzi kutoka kitengo cha utawala nchini humo ambao amepewa na serikali. Anaripoti mwandishi Wetu … (endelea).

Kwenye video ambazo amepakia mitandaoni, Ruto anaonekana akiwa matembezeni na maofisa hao katika makazi yake kabla ya kuketi na kunywa chai pamoja nao.

“Nanywa chai na walinzi wangu wapya, nawakaribisha katika makazi yangu rasmi,” Ruto alisema.

Awali iliripotiwa kuwa Serikali ya Kenya ilimpokonywa Ruto walinzi ambao walikuwa maofisa wa kitengo cha kitengo cha huduma ya jumla (GSU) waliokuwa wakilinda makazi yake yaliyoko Mtaan Karen na Sugoi.

Maofisa hao waliondolewa siku ya Alhamis, Agosti 26, hatua iliyomfanya Ruto kulalamikia usalama wake.

Msemaji wa Ruto, David Mugonyi alisema mabadiliko hayo yalifanywa bila mazungumzo wala makubaliano yoyote.

Mugoyi alisema kamanda wa polisi wa Mtaani Karen alipewa amri kutoka ofisi kuu ikimuagiza kuwaondoa maofisa hao haraka kabla ya muda wa adhuhuri.

Ruto pia amedai kwamba wapinzani wake wanafanya kila wawezalo kuhakikisha wanakamdamiza kabisa kisiasa.

Awali, mfanyakazi wake mkuu Ken Osinde alikuwa amelalamika kwamba walinzi wa Ruto walikuwa wamepunguzwa bila serikali kutoa taarifa yoyote.

Maofisa hao waliondolewa katika kipindi ambacho tofauti baina ya Rais Uhuru Kenyatta na naibu wake zimeonekana hadharani hali ambayo imemfanya Rais kumtaka naibu wake kujiuzulu kama amechoka.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

error: Content is protected !!