Sunday , 5 February 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Mbowe na wenzake, wazidi kuikomalia serikali
Habari za SiasaTangulizi

Mbowe na wenzake, wazidi kuikomalia serikali

Spread the love

KESI ya ugaidi, inayomkabili mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe na wenzake watatu, imepangwa kusikiliza Ijumaa wiki hii. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Mbowe anatuhumiwa kwa kupanga njama na kufadhili ugaidi, ikiwamo kulipua vituo vya mafuta na miundombinu mengine, ambayo haikutajwa na Jamhuri.

Kesi dhidi ya Mbowe na wenzake, inasikilizwa na Jaji wa Mahakama Kuu, Elinaza Luvanda.

Washitakiwa wengine katika kesi hiyo, ni Halfani Bwire Hassan, Adam Kasekwa na Mohammed Abdillah Lingwenya, ambao walikuwa waajiriwa wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

Hata hivyo, usikilizaji wa shauri hilo, hautahusu kesi ya msingi, kufuatia mawakili wa mwanasiasa huyo, wakiongozwa na Peter Kibatala, kuwekea pingamizi hati ya mashitaka.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka mahakamani, Kibatala na wenzake, wamewasilisha mapingamizi matatu, likiwamo hati ya mashitaka kukosa viashiria vya makosa, pamoja na kushitaki watuhumiwa kwa makosa ya kula njama, kinyume na taratibu.

Kupangwa usikilizaji wa shauri hilo kwa siku hiyo, kunatokana na upande wa Jamhuri, kuomba kupatiwa muda, kwa maelezo kwamba hawakujiandaa kushughulikia kwa jambo hilo.

Mapingamizi yaliyowasilishwa leo, yanaeleza kuwa hati ya mashitaka haina hadhi ya kuitwa, “ugaidi.”

Mawakili hao wamewasilisha mifano kadhaa ya mashitaka ya ugaidi, ikiwamo Uganda na Kenya.

Hapo kabla Jaji Luvanda alitupa maombi ya washtakiwa waliotaka shauri hilo lifutwe, kufuatia madai kuwa mahakama hiyo ina mamlaka ya kusikiliza.

Pingamizi hilo liliwasilishwa mahakamani hapo jana tarehe 31 Agosti 2021 na mawakili wa Mbowe na wenzake, wakiongozwa na Kibatala, ambapo wakiiomba mahakama iwaache huru washtakiwa kwa maelezo kuwa haina mamlaka ya kusikiliza mashitaka ya ugaidi.

Mawakili wa upande wa Jamhuri, wakiongozwa na Robert Kidando, walipinga pingamizi hilo wakisema, hoja za upande wa utetezi hazina msingi wa kisheria.

Wakili Kidando, alieleza kuwa tafsiri kwamba mahakama hiyo inasikiliza kesi za makosa ya rushwa na uhujumu uchumi peke yake, sio sahihi.

Alisema, mahakama hiyo ina mamlaka ya kusikiliza mashtaka hayo, baada ya makosa yaliyoko katika sheria ya kuzuia ugaidi, kuwekwa katika Sheria ya Uhujumu Uchumi, kufuatia mabadiliko ya Sheria mbalimbali Na. 3 ya mwaka 2016.

Akataka mahakama hiyo kutupilia pingamizi hilo. Mahakama ya makosa ya uhujumu uchumi, ni sehemu ya Mahakama Kuu.

Naye Wakili wa Serikali Mwandamizi, Nassoro Katuga, alipinga maombi ya washitakiwa kulipwa fidia, akidai kuwa fidia hutolewa endapo mahakama itaona mashitaka yaliyofunguliwa dhidi ya wahusika, yametungwa.

Katika kesi hiyo ya ugaidi Na. 16/2021 yenye mashtaka ya uhujumu uchumi ndani yake, ilianza kutajwa jana mahakamani hapo, baada ya kukamilika kwa taratibu za awali kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Mbowe na wenzake wanashtakiwa kwa makosa sita, ikiwemo la kula njama za kufanya ugaidi; kutaka kudhuru viongozi wa serikali, akiwemo aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya na kufadhili vitendo vya ugaidi, kwa kutoa fedha, ambalo linamkabili kiongozi huyo wa upinzani peke yake.

Wanadaiwa kufanya makosa hayo, kati ya tarehe 1 hadi 5 Agosti mwaka jana, katika maeneo ya mikoa ya Dar es Salaam, Kilimanjaro na Morogoro.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Prof. Muhongo aungana na wananchi ujenzi maabara za sekondari

Spread the loveMBUNGE wa Musoma Vijijini, Profesa Sospeter Muhongo, kwa kushirikiana na...

Habari MchanganyikoTangulizi

Haya hapa majina 12 ya familia moja waliofariki kwenye ajali Tanga

Spread the love  MAJINA 12 kati ya 17 ya waliofariki dunia katika...

Habari za Siasa

CCM apiga marufuku wazazi kuwatumia watoto wa kike kwenye mambo ya kimila

Spread the loveKATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Daniel Chongolo...

Habari za Siasa

Ofisi za mabalozi wa mashina zitumike kuwale vijana kimaadili – Chongolo

Spread the loveKATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo ameagiza...

error: Content is protected !!