Friday , 3 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Halima Mdee amponza Askofu Gwajima bungeni
Habari za Siasa

Halima Mdee amponza Askofu Gwajima bungeni

Halima Mdee
Spread the love

 

MBUNGE wa Singida Magharibi, Elibariki Kingu, ameshangazwa na kitendo cha Chama Cha Mapinduzi (CCM), kutomchukulia hatua Mbunge wake wa Kawe, Askofu Josephat Gwajima, kufuatia makosa yanayomkabili ya kuichonganisha Serikali na wananchi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Akizungumza bungeni jijini Dodoma, leo tarehe 31 Agosti 2021, Kingu amedai kuwa aliyekuwa Mbunge wa Kawe kupitia Chama cha Chadema, Halima Mdee, ambaye kwa sasa ni mbunge viti maalum, hakuwahi kufanya kosa kama hilo.

“Kitendo cha kuwaambia Watanzania kwamba chanjo italeta madhara hii ni hujuma kwa Serikali. Adhabu za Askofu Gwajima zisiishie hapo, hata Mdee hajatufanyia vitimbi namna hii anavyotufanyia Askofu Gwajima. Nashangaa kwa nini CCM mpaka leo hakijamchukulia hatua,” amesema Kingu.

Mbunge huyo wa Singida Magharibi, alitoa kauli hiyo akichangia hoja ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, kuhusu mapendekezo ya adhabu dhidi ya Askofu Gwajima na Mbunge wa Ukonga (CCM), Jerry Silaa, waliokutwa na hatia katika tuhuma zilizokuwa zinawakabili.

Mbali na Kingu, Mbunge Viti Maalum (CCM), Mariam Ditopile, amedai kwamba Askofu Gwajima aliwapa mzigo wakati wa kumnadi katika uchaguzi wa Jimbo la Kawe, mwaka jana, kufuatia mgogoro wake na baadhi ya viongozi wa Kanisa Katoliki.

Ditopile amesema kuwa, wakati wa kampeni CCM ililazimika kuomuombea msamaha ili apate kura.

“Vizuri mmemuita (Askofu Gwajima) mbele ya kamati na ameshindwa kuleta vielelezo. Lakini Kawe kwenye chama chetu waligomeba wengi, viligombea vyama vingi alitupa mzigo mkubwa sana ilibidi twende Kanisa la Romani tufute mambo aliyosema na kwa waislamu,’ amesema Ditopile na kuongeza

“Ili chama kimuamini, arudi kwenye mstari.”

Wabunge hao wa CCM, walikutwa na hatia katika makosa ya kudhalilisha na kushusha hadhi ya Bunge, pamoja na kuwachonganisha wananchi na mhimili huo.

Askofu Josephat Gwajima, Mbunge wa Kawe

Gwajima anadaiwa kutenda kosa kufuatia madai yake ya kwamba baadhi ya viongozi wa Serikali wamepokea hela kumasisha wananchi wachanjwe chanjo ya Ugonjwa wa Korona (UVIKO-19).

Huku Silaa akidaiwa kuwachonganisha wananchi dhidi ya Bunge, baada ya kudai kwamba wabunge hawakatwi kodi katika mishahara yao, kama wananchi wanavyotozwa tozo katika miamala ya simu.

Wabunge hao wamepewa adhabu ya kutoshiriki mikutano miwili mfululizo ya Bunge, pamoja na kupata nusu mshahara katika kipindi wanachotumikia adhabu hiyo.

2 Comments

  • bunge ndo linatakiwa lithibitishie umma kama kweli wanakatwa siyo silaa alithibitishie bunge

  • Unapoona mtoa maoni anaadhibiwa badala ya kujibiwa ujue kuna ukweli wa maoni yake
    Bunge lilitakiwa kujibu na kuthibitisha badala ya kuadhibu watu.
    kwa maoni yangu wameficha ukweli na adhabu hiyo ni kufunga midomo wengine wasiseme.
    kama Mbuge Slaa anafinywa hivyo, nani atasemea wananchi?
    leo hii Mafuta kila mwezi bei juu, huku tozo na hawaoni shida za wananchi.
    Naamini Slaa alikuwa sahihi maana kama haya yangekuwa yanawahusu moja kwa moja wasingeruhusu yatokee

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza uchaguzi mdogo Jimbo la Kwahani

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi, imetangaza uchaguzi mdogo...

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!