May 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Neno la Senzo baada ya kupewa cheo kipya Yanga

Spread the love

 

KAMATI ya utendaji ya klabu ya Yanga, imemteuwa aliyekuwa mshauli Mkuu wa klabu hiyo kwenye masuala ya mabadiliko Senzo Mbatha kuwa mtendaji Mkuu wa muda wa klabu hiyo katika kipindi hiki kabla ya kukamilika kwa mfumo wa mabadilko. Anaripoti Mintanga Hunda, TUDARCo…(endelea)

Senzo ambaye alihudumu nafasi hiyo miaka miwili iliyopita ndani ya klabu ya Simba akitokea nchini Afrika Kusini na kisha baadae kutimkia Yanga na kupewa cheo cha mshauli Mkuu.

Akizungumza na waandishi wa Habari leo Agosti 31, mwaka huu, kwenye makao makuu ya klabu ya Yanga na kusema kuwa majuku aliyonayo sasa ni tofauti na kipindi kile alichokuwa mshauli wa klabu hiyo

“Ahsante kwa nafasi mlionipa mimi kuishauli hii klabu, hili kuhakikisha kila kitu kinaenda sawa, majukumu yangu kwa sasa yatakuwa tofauti na yale niliyokuwa kama mshauli”alisema Senzo

Aidha aliongezea kuwa yupo tayari kwa kukutana na changamoto mpya licha ya kuwa hakuna kilichobadilika kwa kuwa walikuwa wanafanya kazi kama timu mmoja

“Nashukuru kwa msaada wenu mlionipa nipo tayari kwa changamoto hii, na hakuna kilicho badilika kwa kuwa tulikuwa tunafanya kazi kama timu” Aliongezea Senzo

Senzo amepewa cheo hiko mara baada ya mkutano mkuu kupitisha mabadiliko ya uwendeshaji ndani ya klabu hiyo kwa wachama kupiga kura za ndio kwa asilimia 100.

Mkutano huo mkuu wa wanachama wa klabu hiyo ulifanyika Juni 27, mwaka huu kwenye ukumbi wa DYCC na kudhuliwa na mgeni rasmi ambaye ni Rais mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete.

Cheo hiko kipya kinaondoa nafasi ya katibu Mkuu ndani ya klabu hiyo, ambayo ilikuwa inakamiwa na Haji Mfikirwa ambaye anarudi kwenye kamati ya fedha na mipango.

error: Content is protected !!