May 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Tozo miamala ya simu yapunguzwa kwa asilimia 30

Dk. Mwigulu Nchemba, Waziri wa Fedha na Mipango

Spread the love

 

SERIKALI ya Tanzania, imefanya marekebisho ya tozo za miamala ya simu, kwa kupunguza viwango vyake kwa asilimia 30. Anaripoti Mwanaharusi Abdallah, TUDARCo … (endelea).

Pia wamiliki wa makampuni ya simu wameridhia kupunguza kwa asilimia 10 viwango vya tozo za miamala kati ya mtandao mmoja na mtandao tofauti.

Taarifa hiyo imetolewa leo Jumanne, tarehe 31 Agosti 2021 na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano cha Wizara ya Fedha na Mipango, Benny Mwaipaja.

Taarifa ya Mwaipaja imesema kuwa, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Mwigulu Nchemba, leo amesaini marekebisho ya kanuni za tozo hiyo, ambayo yamepunguza viwango vyake.

“Katika kutekeleza maelekezo ya Rais Samia Suluhu Hassan, ya kupitia upya tozo za miamala ya simu, Dk. Mwigulu leo ametia saini marekebisho ya Kanuni za Tozo za Miamala ya Kielektroniki za Kutuma na Kutoa Fedha za Mwaka 2021,” imesema taarifa ya Mwaipaja.

Taarifa ya Mwaipaja imesema “na kupunguza viwango vya tozo za miamala hiyo na kupunguza viwango vya tozo za miamala hiyo kwa asilimia 30.”

Aidha, taarifa ya Mwaipaja imesema, Serikali imefanya majadiliano na watoa huduma za simu ambao nao wameridhia kupunguza viwango vya tozo hiyo kati ya mtandao mtandao na mtandao mwingine, kwa asilimia 10.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, viwango vya tozo vilivyopunguzwa vitatangazwa kesho tarehe 1 Septemba 2021, katika tangazo la Serikali.

Serikali inaamini kuwa, uamuzi huo utatoa nafuu kwa wananchi na kuiwezesha Serikali kupata fedha za kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kama ilivyokusudiwa wakati tozo hizo ziliporidhiwa na kupitishwa na Bunge la Bajeti la 2021/2022,” imesema taarifa ya Mwaipaja.

Kwa mujibu wa tozo hizo zilizoanza kutozwa na Serikali kuanzia tarehe 15 Julai 2021, mteja alikuwa anakatwa kati ya Sh. 10 hadi 10,000 kulingana na kiasi cha muamala husika wa kutoa au kutuma fedha.

error: Content is protected !!