Saturday , 20 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Taliban washerehekea Wamarekani kuondoka Afghanistan
Kimataifa

Taliban washerehekea Wamarekani kuondoka Afghanistan

Spread the love

 

MILIO ya risasi ya sherehe ilisikika kote jijini Kabul chini Afghanistan leo Jumanne tarehe 31 Agosti 2021, wakati wapiganaji wa Taliban walipodhibiti uwanja wa ndege wa Kabul kabla ya alfajiri, kufuatia kuondoka kwa wanajeshi wa mwisho wa Marekani. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Kuondoka huko kunashiria kumalizika kwa vita vya miaka 20 ambavyo viliwaacha wanamgambo wa Kiislam wakiwa na nguvu kuliko ilivyokuwa mwaka wa 2001.

Picha za video zilizosambazwa na Taliban zilionyesha wapiganaji wakiingia kenye uwanja huo wa ndege baada ya wanajeshi wa mwisho wa Marekani kuondoka kwa ndege ya C-17 dakika moja kabla ya usiku wa manane, katika kile kinachotajwa na baadhi ya wachambuzi kama kisa cha aibu kwa Marekanin na washirika wake wa NATO.

“Ni siku ya kihistoria na wakati wa kihistoria,” msemaji wa Taliban, Zabihullah Mujahid aliwaambia waandishi wa habari katika uwanja wa ndege baada ya kuondoka kwa Wamarekani.

“Tunajivunia nyakati hizi, kwamba tuliikomboa nchi yetu kutoka kwa nchi zenya nguvu kubwa,” aliongeza.

Picha kutoka Pentagon ilionyesha mwanajeshi wa mwisho wa Marekani akiingia ndani ya ndege ya mwisho ya uokoaji kutoka Kabul.

Vita hivyo nchini Afghanistan ndivyo vya muda mrefu zaidi kwa Marekani, vikigharimu takriban dola trilioni mbili, na vilimalizika kwa wanamgambo wenye msimamo mkali wa Kiislam kudhibiti eneo zaidi kuliko wakati wa utawala wao uliopita.

Zaidi ya watu 123,000 wameondoka nchini humo kwa kuhofia utawala wa Taliban.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

Habari MchanganyikoKimataifa

Tetemeko la ardhi laua 7, lajeruhi 800 Taiwan

Spread the loveWatu wapatao saba wamefariki dunia na wengine zaidi ya 800...

error: Content is protected !!