Tuesday , 7 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mbowe, wenzake waweka pingamizi kesi ya ugaidi
Habari za SiasaTangulizi

Mbowe, wenzake waweka pingamizi kesi ya ugaidi

Spread the love

 

MAWAKILI wanaomtetea Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake, katika kesi ya kula njama za kufanya ugaidi, wameweka pingamizi kwa Mahakama Kuu ya Tanzania, Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, kusikiliza kesi hiyo kwa madai kwamba haina mamlaka. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Mbowe na wenzake wameipinga mahakama hiyo kuwa haina mamlaka ya kusikiliza kesi yao kwa mashtaka ya ugaidi na kwamba kwa mujibu wa Sheria ya Kuzuia Ugaidi kesi yao inapaswa kusikilizwa na Mahakama Kuu ya kawaida na si hiyo ambayo ni Divisheni Maalum.

Katika kesi hiyo ya uhujumu uchumi Na. 16/2021, Mbowe na wenzake anashtakiwa kula njama za kufanya ugaidi, kufadhili ugaidi sambamba na kulipua vituo vya mafuta ilianza kusikilizwa leo baada ya kuhamishiwa katika mahakama hiyo, ikitokea katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam.

Mbali na Mbowe, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni, Halfani Bwire Hassan, Adam Kasekwa na Mohammed Abdillah Lingwenya.

Jopo la mawakili upande wa utetezi, ukiongozwa na Wakili Peter Kibatala, umeweka pingamizi hilo, ikidai kwamba mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza mashtaka ya ugaidi, kwa mujibu wa Sheria ya Kuzuia Ugaidi.

Akiwasilisha pingamizi hilo, Wakili Kibatala amedai kesi hiyo ilipaswa kusikilizwa na Mahakama Kuu ya Tanzania na sio katika mahakama ya divisheni maalum.

Katika mapingamizi hayo, Mawakili wa Mbowe, wanaomba washtakiwa waachwe huru na walipwe fidia ya gharama walizotumia kuendesha kesi hiyo.

Hata hivyo, Mawakili upande wa Jamhuri wamepinga pingamizi hilo, ukidai kwamba hoja zake si sahihi kwa mujibu wa sheria.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Robert Kidando alidai kwamba tafsiri ya kwamba mahakama hiyo inasikiliza kesi za makosa ya rushwa na uhujumu uchumi peke yake, sio sahihi.

Akidai mahakama hiyo ina mamlaka ya kusikiliza mashtaka hayo, baada ya makosa yaliyoko katika sheria ya kuzuia ugaidi, kuwekwa katika Sheria ya Uhujumu Uchumi, kufuatia mabadiliko ya sheria mbalimbali Na. 3 ya 2016.

Wakili Kidando ameiomba mahakama hiyo itupilie mbali pingamizi hilo, kwa madai kwamba ina mamlaka ya kusikiliza mashtaka ya ugaidi, kwa sababu ni sehemu ya Mahakama Kuu ya Tanzania.

Naye Wakili wa Serikali Mwandamizi, Nassoro Katuga alipinga maombi ya washtakiwa kulipwa fidia, akidai kwamba fidia hutolewa endapo mahakama itaona mashtaka yaliyofunguliwa dhidi ya washtakiwa husika, ni ya kutungwa.

Baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili, Jaji Luvanda aliahirisha usikilizwaji wa kesi hiyo, hadi kesho Jumatano, tarehe 1 Septemba 2021, ambapo mahakama hiyo itatoa uamuzi wa pingamizi hilo.

Mbowe na wenzake wanashtakiwa kwa mashtaka sita, ikiwemo la kula njama za kufanya ugaidi na shtaka la kutaka kudhuru viongozi wa Serikali, akiwemo aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya,  yanayowakabili wote,

Na shtaka la kufadhili vitendo vya ugaidi kwa kutoa fedha za kufadhili ugaidi, linalomkabili Mbowe peke yake.

Washtakiwa hao wanadaiwa kufanya makosa hayo kati ya tarehe 1 hadi 5 Agosti 2021, katika maeneo ya mikoa ya Dar es Salaam, Kilimanjaro na  Morogoro.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Jacob, Malisa wapandishwa kizimbani kwa mashtaka ya uongo mitandaoni

Spread the loveMKURUGENZI wa Shirika la Haki, Godlisten Malisa na mwanachama wa...

BiasharaHabari za Siasa

Bunge laitaka Serikali kudhibiti ufisadi miradi ya mkakati

Spread the loveKAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, imeitaka Serikali kuimarisha...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Wizara ya Uchukuzi yaomba kuongezewa bajeti na Bunge

Spread the loveWIZARA ya Uchukuzi imeliomba Bunge liidhinishe bajeti yake kwa mwaka...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Serikali kutafuta mwekezaji mwingine Bandari ya Dar es Salaam

Spread the loveSERIKALI inaendelea kutafuta mwekezaji mwingine atakayeendesha gati namba nane hadi...

error: Content is protected !!