Friday , 3 February 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Zitto aomba ushirikiano ukaguzi vitabu vya TCD
Habari za Siasa

Zitto aomba ushirikiano ukaguzi vitabu vya TCD

Spread the love

 

MWENYEKITI wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD), Zitto Kabwe amekiomba Kituo cha sheria na Haki za binadamu (LHRC) kusaidia kupata mkaguzi wa hesabu kufanya ukaguzi Maalumu wa vitabu vya TCD. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Zitto amesema taasisi hiyo haijawahi kukaguliwa hesabu zake tangu mwaka 2016.

Zitto ametoa ombi hilo mapema wiki hii alipotembelea wadau muhimu wa demokrasia nchini ikiwemo vyama vya siasa na taasisi za kiraia.

Zitto ambaye hivi karibuni amekabidhiwa mikoba ya uenyekiti wa TCD amesema hatua hiyo ni mojawapo mbinu ya kuifufua TCD ili kuhakikisha fedha za taasisi hiyo zinatunzwa vizuri na kutumika kwa malengo stahiki.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa LHRC, Anna Henga alisema taasisi yake imeitikia wito huo na kuahidi kufanyia kazi haraka iwezekanavyo.

“Tumefurahishwa na mwenendo wa kazi za TCD na tuko tayari kuendelea kuwawezesha kwenye suala la kufanya ukaguzi wa vitabu, tutashirikiana kuhakikisha tunalifanyia kazi mapema.”

Aidha, Taasisi ya Foundation for Civil Society (FCS), kwa upande wao waliahidi kufanya kazi na TCD katika kuandaa mkutano mkubwa wa Haki, Amani na Maridhiano unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa Septemba mwaka huu.

Dhumuni la mkutano huo ni kuanza mchakato wa majadiliano ya kisiasa kwa lengo la kutatua changamoto za demokrasia zinazokabili Tanzania sasa.

Wakati taasisi ya Legal Services Facility (LSF) kupitia  Mkurugenzi Mkuu, Luku Ng’wanakilala aliahidi kufanya kazi na TCD katika eneo la nafasi ya wanawake katika uongozi wa vyama vya Siasa.

Zitto alianza ziara ya kutembelea wadau na vyama wanachama wa TCD baada ya kiteuliwa kuwa mmwenyekiti mpya TCD Tarehe 26 mwezi Agosti.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

ACT-Wazalendo yaiangukia Serikali kunusuru wananchi Liwale, Nachingwea

Spread the love  CHAMA cha ACT-Wazalendo, kimeitaka Serikali kuchukua hatua za haraka...

Habari za SiasaTangulizi

Vigogo wanaokwamisha mradi Liganga na Mchuchuma kitanzani

Spread the love  NAIBU Spika wa Bunge, Mussa Zungu, watu wanaokwamisha utekelezaji...

Habari za Siasa

Gridi ya Taifa kufumuliwa kukabiliana na katizo la mgao wa umeme

Spread the love  WAZIRI wa Nishati, Januari Makamba, amesema Serikali ina mpango...

Habari za Siasa

Kamati ya Bunge yaitaka Serikali kuchunguza dawa za asili

Spread the love  KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo...

error: Content is protected !!