Friday , 29 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Utafiti wa vinasaba (DNA) kwa makabila yote waja
Habari Mchanganyiko

Utafiti wa vinasaba (DNA) kwa makabila yote waja

Spread the love

 

WATAFITI na wanataaluma wa vinasaba nchini  wamesema kuna uhitaji mkubwa ufanyikaji wa utafiti za vinasaba vya binadamu ili kubaini vyanzo mbalimbali vya magonjwa na kutambua uhalisia wake ili kurahisisha namna sahihi ya upatikanaji wa tiba zake. Anaripoti Glory Massamu- TUDARCo … (endelea).

Wakizungumza leo tareehe 31, Agosti 2021, jijini Dar es Salaam katika mkutano huo wa kwanza wa wataalam kutoka chama cha wanataaluma wa vinasaba wamesema matumizi ya tafiti ni muhimu hususani katika kipindi hiki ambacho kuna ongezeko kubwa la magonjwa adimu.

Mkutano huo umelenga kuhamasisha watunga sera na maamuzi katika kuwalenga waathirika wa magonjwa adimu.

Mwanzilishi wa taasisi ya magonjwa adimu, Shamsa Mbaraka ambaye pia ni mtalaam wa magonjwa adimu alisema kutokana na baadhi ya magonjwa kuonekana kuathiri zaidi watu katika baadhi ya maeneo fulani, sasa wameandaa mchakato wa kufanya tafiti za vinasaba kwa wawakilishi kutoka makabila mbalimbaali ili kupata taarifa juu ya vinasaba na magonjwa ya makabila husika.

Makamu mwenyekiti wa Taasisi ya vinasaba Tanzania, Dk. Kilaza Samson alisema utafiti wa vinasaba uinatoa picha halisi ya magonjwa na namna ya kuyatibu.

Hata hivyo Profesa Raphaeli Sangeda kutoka Idara ya Phamasia amesema kuwa kuna umuhimu wa elimu nasaha kwa wataalamu wa afya pamoja na wanajamii kuhusu umuhimu wa tafiti za vinasaba.

Pia ameiomba serikali kusaidia vifaa tiba ili kuwezesha utafiti huo pamoja na hatimiliki ya teknolojia.

Wakati Mwakilishi Mamlaka ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Ally Kanenda alisema sayansi ya vinasaba kwenye tiba ambayo inatajwa kama tawi jipya la tiba, nchi zinazoendelea huangazia uhusiano uliopo kati ya vinasaba katika mwili wa binadamu na mazingira.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Puma Energy Tz: Watanzania tudumishe amani kuvutia uwekezaji

Spread the loveKAMPUNI ya Mafuta ya Puma Tanzania imewakutanisha wadau mbalimbali katika...

Habari Mchanganyiko

DAWASA waanza utekelezaji agizo la Samia

Spread the loveMamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam...

Habari MchanganyikoKimataifa

Zuma akataliwa kugombea urais

Spread the loveTUME Huru ya Uchaguzi Afrika Kusini (IEC) imemwondoa rais wa...

Habari Mchanganyiko

Mtandao watetezi wa haki za mazingira Tanzania waundwa

Spread the loveMTANDAO wa watetezi wa haki za mazingira nchini Tanzania, umeundwa...

error: Content is protected !!