Tuesday , 7 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Simba wauwa Wanafunzi watatu Arusha
Habari Mchanganyiko

Simba wauwa Wanafunzi watatu Arusha

Spread the love

 

WANAFUNZI watatu wa Shule ya Msingi Ngoile wilayani Ngorongoro, Mkoa wa Arusha, wameuawa kwa kushambuliwa na Simba, walipokuwa wanatafuta mifugo yao iliyopotea porini. Anaripoti Mwandishi Wetu, Arusha … (endelea).

Taarifa ya tukio hilo imetolewa leo Alhamisi, tarehe 5 Agosti 2021 na Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha, Justine Masejo, akizungumza na wanahabari.

Kamanda Masejo amesema, wanafunzi hao ambao ni Olobiko Metui (10), Ndaskoi Sangu (9) na Sanka Saning’o (10), waliuawa tarehe 3 Agosti mwaka huu.

Amesema wanafunzi hao waliokuwa darasa la tatu, walienda porini kuitafuta mifugo hiyo, wakitokea nyumbani kwao baada ya kurudi kutoka shule.

Kamanda Masejo amesema, mwanafunzi mmoja, Kiambwa Lektony (11), alifanikiwa kutoroka katika mashambulizi ya Simba, ambaye anapatiwa matibabu katika Zahanati ya Kata ya Olbalbal, mkoani humo.

“Miili ya marehemu wote imefanyiwa uchunguzi wa kidaktari na imeshakabidhiwa kwa ndugu zao kwa ajili ya mazishi,” amesema Kamanda Masejo.

Kamanda Masejo amewataka wafugaji wasiwape watoto majukumu ya kuchunga mifugo, hasa katika maeneo ya vijiji vinavyopakana na hifadhi za wanayamapori, ili kuokoa maisha yao.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mahakama yatoa uamuzi zuio dhidi ya Club House

Spread the loveMAHAKAMA Kuu ya Tanzania, Masjala Kuu jijini Dar es Salaam,...

Habari Mchanganyiko

GGML, OSHA yawanoa bodaboda 200 Arusha

Spread the loveZAIDI ya madereva bodaboda 200 wa jiji la Arusha wamepatiwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Serikali kuwakopesha wajasiriamali 18.5bn/- kupitia NMB

Spread the loveSerikali imetenga kiasi cha Sh 18.5 bilioni kwa ajili ya...

AfyaHabari Mchanganyiko

Huduma za kibingwa zazinduliwa katika hospitali za halmashauri 184

Spread the loveSERIKALI imezindua huduma za matibabu za kibingwa katika hospitali 184...

error: Content is protected !!