January 17, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mbowe afikishwa Kisutu, ulinzi waimalishwa

Freeman Mbowe na wenzake wakiwa mahakamani Kisutu

Spread the love

 

KIONGOZI wa chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania cha Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu, wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Mbowe na wenzake; Halfani Bwire Hassan, Adam Hassan Kasekwa na Mohammed Abdillahi Lingwenya, wamefikishwa mahakamani hapo mapema leo asubuhi Ijumaa, tarehe 6 Agosti 2021.

Ni baada ya jana Alhamisi, kesi hiyo ilishindwa kuendelea kwa njia ya mtandao ‘video conference’ kusumbua hivyo Hakimu Mwandamizi, Thomas Simba anayesikiliza kesi hiyo, kutoa amri ya washtakiwa hao kufikishwa mahakamani.

Tayari Mbowe na wenzake wamekwisha fikishwa katika chumba cha mahakama.

Kama ilivyokuwa jana Alhamisi, ulinzi umeimalishwa na leo ni zaidi kwani baadhi ya viongozi wa Chadema wanazuiwa kuingia mahakamani.

Askari kazu na waliovalia sare, wameizunguka mahakama hiyo na wengine wamesimama juu ya mahakama hiyo.

Baadhi ya viongozi walioingia ni; Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika, Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia.

Endelea kufuatilia MwanaHALISI TV, MwanaHALISI Online na mitandao yetu ya kijamii kwa habari na taarifa mbalimbali

error: Content is protected !!