Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Marekebisho VAT ya Tanzania, Zanzibar kufanyika 2021/22
Habari Mchanganyiko

Marekebisho VAT ya Tanzania, Zanzibar kufanyika 2021/22

Dk. Mwigulu Nchemba, Waziri wa Fedha na Mipango
Spread the love

 

WAZIRI wa Fedha na Mipango wa Tanzania, Dk. Mwigulu Nchemba, amependekeza marekebisho ya Sheria ya Kodi ya Ongezeko la Thamani ili kurudisha utaratibu wa kurejesha VAT kwa bidhaa zinazonunuliwa Tanzania Bara na kutumika Tanzania Zanzibar. Anaripoti Jemima Samwel, DMC…(endelea).

Akiwasilisha Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2021/22, leo Alhamis bungeni jijini Dodoma, Dk. Mwigulu amesema, hii inatokana na mfumo wa kutoza VAT kwa kiwango cha asilimia sifuri kwa bidhaa za viwandani pekee kutowanufaisha wafanyabiashara wa Zanzibar wanaonunua bidhaa na kutozwa VAT Tanzania Bara na kutozwa tena VAT bidhaa hizo zinapopelekwa Zanzibar.

“Aidha, inapendekezwa marejesho ya VAT yatakayofanyika kwa bidhaa zinazotoka Tanzania Bara kwenda Zanzibar yafanyike pia kwa bidhaa zitakazotoka Zanzibar kwenda Tanzania Bara sambamba na marekebisho ya vifungu husika vya Sheria za VAT kwa pande zote mbili za muungano.”

“Ili kuwa na ufanisi wa marejesho, maboresho ya mifumo yatafanyika ili isomane baina ya Tanzania Bara na Zanzibar,” amesema Dk. Mwigulu na kuongeza:

“Kutokana na utaratibu huu, kiwango cha asilimia sifuri ya Kodi ya Ongezeko la Thamani kilichokuwa kinatozwa bidhaa hizo kitasitishwa.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari Mchanganyiko

Chongolo aonya viongozi vijiji kutouza NIDA kwa wageni

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amewaonya viongozi wa...

error: Content is protected !!