May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Nyasi bandia zapata msahama wa Kodi

Spread the love

 

Waziri wa Fedha na Mipangango Mwigulu Nchemba amesema kuwa katika bajeti ya mwaka 2021/22 watasamehe ongezeko la kodi la thamani (VAT) kwa nyasi bandia kwa ajili ya marekebisho kwenye viwanja vibovu ili kukuza mchezo wa soka. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Mwigulu amesema hay oleo bungeni tarehe 1o Juni, 2021 wakati akiwasilisha bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2021/22.

Katika eneo hilo Waziri Mwigulu amesema kuwa viwanja vingi vya michezo nchini ni vibovu kiasi cha kupelekea baadhi ya timu kama Yanga kutopata matokeo katika michezo ya mikoani.

“Viwanja vyetu vingi nchini ni vibovu na vinasababisha timu bora kama Yanga ikienda mikoani inashindwa kupata matokeo.” Alisema Mwigulu

Dk. Mwigulu Nchemba, Waziri wa Fedha na Mipango

Aidha Waziri huyo aliongezea kuwa msamaha huo kwa kodi ya ongezeko la thamani kwa nyasi hizo zitausisha kwa viwanja vya mpira vilivyopo kwenye majiji.

“Napendekeza kusamehe kodi la ongezeko la thamani kwa nyasi za bandia, kwa ajili ya viwanja vya mpira vilivyopo kwenye Majiji na msahama huo utahusisha ridhaa kutoka kwenye Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).” Aliongezea Mwigulu

Serikali imeamua kuchukua hatua hiyo, kwa ajili ya kuendeleza michezo nchini, kwa kuwa na miundombinu bora kwenye sekta hiyo, ambapo kilikuwa kilio cha wadau kwa muda mrefu.

error: Content is protected !!