Friday , 3 February 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Bajeti 2021/22 kuzipa pumzi NGO’s
Habari Mchanganyiko

Bajeti 2021/22 kuzipa pumzi NGO’s

Spread the love

 

BAJETI Kuu pendekezwa ya Serikali ya Tanzania, kwa mwaka wa fedha wa 2021/22, imekuja na mikakati ya kuzipa nafuu Taasisi Zisizo za Kiserikali (NGO’s), ikiwemo kusamehe kodi ya ongezeko la thamani (VAT), kwenye bidhaa na huduma za miradi inazotekeleza. Anaripoti Nasra Bakari, DMC…(endelea).

Hyao yamesemwa leo Alhamisi, tarehe 10 Juni 2021 na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Mwigulu Nchemba, akiwasilisha mapendekezo ya Bajeti Kuu ya Serikali kwa 2021/22, bungeni jijini Dodoma.

“Napendekeza Kutoa msamaha wa kodi ya ongezeko la thamani, kwa NGO’s, kwenye bidhaa na huduma zitakazotumika kwenye miradi inayotekelezwa na taasisi husika,”

“Aidha, taasisi zitakazonufaika na msamaha huo, ni zile ambazo zina mikataba na Serikali, yenye kipengele kinachotoa msamaha wa kodi ya ongezeko la thamani,” amesema Dk. Mwigulu.