Thursday , 2 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Ndugai aomba Rais Samia aitishe mkutano wa wanaume
Habari za SiasaTangulizi

Ndugai aomba Rais Samia aitishe mkutano wa wanaume

Spread the love

 

SPIKA wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai, amemwomba Rais wa nchi hiyo, Samia Suluhu Hassan, kufanya kikao maaluma na wanaume pekee. Anaripoti Jemima Samwel, DMC … (endelea).

Ni baada ya Rais Samia, kufanya kikao na wanawake wa Mkoa wa Dodoma, juzi Jumanne tarehe 8 Juni 2021, katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete.

Mkutano huo, ulihudhuliwa na wanawake mbalimbali wakiwemo wabunge na watumishi wa Bunge wote wanawake.

Kuhudhulia kwa wanawake wabunge kwenye mkutano huo, kulifanya kikao cha Bunge la Jumanne asubuhi, kuhudhuliwa na wabunge wanaume pekee.

Leo Alhamisi, tarehe 10 Juni 2021, mara baada ya kipindi cha maswali na majibu kumalizika, Mbunge wa Nyangw’ale (CCM), Hussein Amar alisimama kuomba mwongozo wa kiti cha Spika, kilichokuwa kikiongozwa na Job Ndugai.

Ameanza kwa kusema, hivi karibuni kulitokea jambo humu ndani la kuhusiana na mavazi, “kwa sasa unaona tunapendeza.”

“Nawaomba wabunge kina mama watusaidie huko kwenye majimbo, kuwa na madawati ya kuwasaidia kina baba kupeleka malalamiko yao,” amesema mbunge huyo akisema, suala hilo ni muhimu kwani wapo wanaume wanaokutana na ukatili ila hawana pa kuyapeleka.

Mara baada ya kumaliza, alismama Spika Ndugai na kusema, “mbunge unachokoza nyuki, kina mama ni jeshi kubwa. Juzi tu walituacha peke yetu tukateteleka.”

Huku wabunge wakifurahia, Spika Ndugai akasema “japo nilijaribu kutengeneza njama ili tupitishe sheria haraka haraka, nikaogopa kwamba tunaweza kumaliza hapa bungeni ikaishia dawatini kwa Rais.”

Kuhusu hoja ya Amar ya madawati ya wanaume, Spika Ndugai amesema “kwa kweli panahitajika dawati la wanaume mahali, kweli kabisa, tukienda kwa namna hii tukaona ni sawa, hapana, wakabaki kugugumia tu., wanawake tuwasaidie wanaume wapo wanaonyanyasika kweli.”

“Lakini tunaomba Rais aite mkutano wa wanaume tu,” amesema Spika Ndugai.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza uchaguzi mdogo Jimbo la Kwahani

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi, imetangaza uchaguzi mdogo...

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!