Wednesday , 8 February 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Bajeti 2021/22 EAC kuwasilishwa Leo
Habari za SiasaTangulizi

Bajeti 2021/22 EAC kuwasilishwa Leo

Dk. Mwigulu Nchemba, Waziri wa Fedha na Mipango
Spread the love

 

LEO Alhamisi, tarehe 10 Juni 2021, nchini za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), zitawasilisha Bajeti za nchi zao, ikiwemo Tanzania. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Ni utaratibu waliojiwekea nchi za EAC ambazo ni; Uganda, Kenya, Tanzania, Burundi, Rwanda na Sudan Kusini kuwasilisha bajeti zake siku moja.

Nchini Tanzania, Waziri Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Mwigulu Nchemba, atawasilisha Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2021/22, katika Bunge jijini Dodoma.

Awali, saa 4:00 asubuhi ya leo, Dk. Mwigulu atawasilisha Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2020 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka 2021/2022.

Bunge la Tanzania

Hii itakuwa Bajeti ya kwanza ya Serikali ya awamu ya sita, chini ya Rais wake, Samia Suluhu Hassan ambaye aliingia madarakani tarehe 19 Machi 2021.

Ni baada ya kifo cha aliyekuwa Rais John Pombe Magufuli, aliyefariki dunia tarehe 17 Machi 2021, katika Hospitali ya Mzena, iliyopo Makumbusho, mkoani Dar es Salaam na mwili wake, kuzikwa nyumbani Chato, Mkoa wa Geita, 26 Machi 2021.

Endelea kufuatilia MwanaHALISI TV, MwanaHALISI Online na mitandao yetu ya kijamii kwa habari na taarifa mbalimbali.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Bunge labaini madudu mfumo ukusanyaji mapato, h’shauri tatu kikaangoni

Spread the love  KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali...

Habari za Siasa

Mkuu wa wilaya ya Rungwe azindua vyumba sita vya madarasa vya thamani ya 64 mil

Spread the love  MKUU wa Wilaya ya Rungwe, Jaffar Haniu amezindua vyumba...

Habari za Siasa

Mbunge afurahia mabilioni ya Samia kutua jimboni

Spread the love  MBUNGE wa Igunga, Nicholas Ngassa ameishukuru Serikali kwa utekelezaji...

Habari za Siasa

PIC yaishauri Serikali kuanzisha mfuko wa uwekezaji kusaidia mashirika ya umma

Spread the love  KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji...

error: Content is protected !!