Tuesday , 7 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Ubadhirifu wa Bil 1.67, wang’oa vigogo 11 wizara ya fedha
Habari za SiasaTangulizi

Ubadhirifu wa Bil 1.67, wang’oa vigogo 11 wizara ya fedha

Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu wa Tanzania
Spread the love

 

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa, amewasimamisha kazi vigogo 11 wa Wizara ya Fedha na Mipango, ili kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazowakabili, za matumizi mabaya ya fedha za umma. Anaripoti Nasra Bakari, DMC … (endelea).

Waziri Majaliwa aliwasimamisha kazi vigogo hao, jana tarehe 27 Mei 2021, katika kikao kazi kati yake na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Mwigulu Nchemba, pamoja na watendaji wa wizara hiyo, kilichofanyika jijini Dodoma.

Vigogo waliosimamishwa ni, Mkaguzi Mkuu, Mkaguzi Msaidizi na watendaji wengine tisa wa wizara hiyo, akiwemo Christopher Mkupama, Mtobesi Matike, Denis Kanza, Alike Mwakitekele, Tumaini Mwakalange na Fredrick Mushi.

Waziri Majaliwa alisema, watendaji hao wanadaiwa kufanya matumizi mabaya ya fedha za umma zaidi ya Sh. 1.67 bilioni, katika kipindi cha miezi mitatu, kuanzia Machi hadi Mei 2021.

Kufuatia ubadhirifu huo, Waziri Majaliwa,alimuagiza Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (Takukuru), Salum Hamduni, kufanya uchunguzi dhidi ya tuhuma hizo.

“Sio utaratibu mzuri wa matumizi ya fedha, lazima tuseme ukweli. Hatuwezi kutumia fedha kwa kiwango hiki, tena ni miezi mitatu. Kwa hiyo mkurugenzi mkuu fanya uchunguzi wa kina, wa haya malipo mbalimbali ya fedha ndani ya wizara hii,” alisema Majaliwa.

Waziri Majaliwa alitaja matumizi hayo ya fedha kuwa ni, malipo yaliyofanyika tarehe 31 Machi mwaka huu, kupitia vocha namba 30 ya Sh. 251 milioni, kwa maelezo kwamba ni malipo maalum, bila kutaja kazi iliyofanyika.

Matumizi mengine ni, Sh. 198.8 milioni, yaliyofanyika tarehe hiyo hiyo, kwa madai kuwa ni posho ya honoria.

“Tarehe 31 Machi 2021, Sh. 251 milioni imelipwa kwa kazi maalum, haijaelezwa kwa kazi gani. waliofanya kazi wenyewe hawaonekani. Hebu tuangalie , kwa siku wewe una kazi maalum ya kujilipa posho hiyo.

Kwa hali ya kawaida nyie wote ni watumishi wa umma, hizo kazi zenu mlizopewa unajilipa Sh. 251 milioni kwa kazi malaum, labda makatibu wakuu mtatuambia kazi gani mliyonayo kujilipa Sh. 252 milioni kwa siku moja,” alisema Majaliwa.

Baadhi ya Maofisa wa Wizara ya Fedha na Mipango

Tarehe 8 Aprili 2021, wizara hiyo iliwalipa watumishi 27 kiasi cha Sh. 44.5 milioni, kwa ajili ya posho ya kazi maalum ya wiki nne.

Tarehe 13 Aprili mwaka huu, zilitumika Sh. 155.2 milioni, kulipa watumishi 68, kwa ajili ya posho maalum ya kazi ya wiki tatu.

Pia, tarehe 30 Aprili 2021, wizara hiyo ilitoa fedha mara tatu kwa ajili ya matumizi mbalimbali, ikiwemo Sh. 43.9 milioni kwa ajili ya kuandaa mpango wa kuhifadhi mazingira, Sh. 14.4 milioni kwa ajili ya siku ya wanawake na Sh. 43. Na kufanya wizara hiyo kutumia jumla ya Sh. 101.8 milioni.

Waziri Majaliwa alisema, tarehe 1 Mei 2021, wizara hiyo ililipa Sh. 184.1 milioni na Sh. 264 milioni, kwa ajili ya malipo ya kazi maalum.

Tarehe 3 Mei 2021, wizara ililipa Sh. 146.5 milioni kwa watumishi 125 , kwa ajili ya malipo ya kuandaa mpango kazi wa manunuzi. Pamoja na Sh. 171.2 milioni kwa ajili ya kuandaa nyaraka za bunge.

Majaliwa alisema, wizara hiyo ililipa Sh. 155 milioni, kwa baadhi ya watumishi ikiwa ni posho ya kuandaa miongozo ya kazi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Jacob, Malisa wapandishwa kizimbani kwa mashtaka ya uongo mitandaoni

Spread the loveMKURUGENZI wa Shirika la Haki, Godlisten Malisa na mwanachama wa...

BiasharaHabari za Siasa

Bunge laitaka Serikali kudhibiti ufisadi miradi ya mkakati

Spread the loveKAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, imeitaka Serikali kuimarisha...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Wizara ya Uchukuzi yaomba kuongezewa bajeti na Bunge

Spread the loveWIZARA ya Uchukuzi imeliomba Bunge liidhinishe bajeti yake kwa mwaka...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Serikali kutafuta mwekezaji mwingine Bandari ya Dar es Salaam

Spread the loveSERIKALI inaendelea kutafuta mwekezaji mwingine atakayeendesha gati namba nane hadi...

error: Content is protected !!