Friday , 3 May 2024
Home Kitengo Michezo Manchester United, Villarreal kuminyana fainali Euroa leo
Michezo

Manchester United, Villarreal kuminyana fainali Euroa leo

Spread the love

 

Manchester United leo itashuka dimbani kumenyana na Villarreal kwenye fainali ya kombe la Europa ambao itapigwa kwenye dimba la Gudansk nchini Poland nchini Poland majira ya saa 4 usiku. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Villarreal ambao wanashika nafasi ya saba kwenye msimao wa La Liga wanaingia kwenye fainali hiyo mara baada ya kuwaondosha Arsenal kwenye hatua ya nusu fainali, huku Manchester United ikitinga fainali mara baada ya kuitoa klabu ya As Roma kwa jumla ya mabao 8-5, katika michezo yote miwili.

Kwenye fainali ya michuano hiyo timu za kutoka nchini England zimekuwa hazipati matokeo mazuri kutoka kwa timu zinazotoka nchini Hispania ambapo mara ya mwisho timu iliyopata matokeo kwenye fainali nchini England ilikuwa Liverpool kwenye masimu wa 2000/01 ambapo waliwafunga Alves.

Kuanzia hapo timu hizo kutoka Ligu Kuu nchini England zilipata wakati mgumu mbele ya timu kutoka La Liga ambapo Sevilla alimfunga Middlesbrough, Atletico Madrid ilibuka na ushindi dhidi ya Fulham na hivi karibuni mwaka 2016 Sevilla iliifunga Liverpool.

Manchester United inaingia kwenye mchezo huo wa fainali huku ikiwa na kumbukumbu ya kutwaa taji hilo kwenye fainali yake ya mwisho waliocheza tarehe 24 Mei, 2017 dhidi ya Ajax na kuibuka na ushindi wa mabao 2-0.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Europa na Conference kukupatia pesa ndefu leo

Spread the love  ALHAMISI ya leo tutaenda kushuhudia mitanange ya kukata na...

Habari MchanganyikoMichezo

Wanamichezo Mei Mosi wachangia wahitaji vitu vya mil. 11.5

Spread the loveWanamichezo wanaoshiriki Michezo ya Mei Mosi Taifa 2024 jijini Arusha...

Michezo

Usiku wa Ulaya umerejea kibabe kabisa

Spread the love  LIGI ya Mabingwa barani Ulaya imerejea tena na awamu...

Habari MchanganyikoMichezo

Mambo ya Ndani, Ulinzi zang’ara michezo ya Mei Mosi Arusha

Spread the loveRais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini (TUCTA), Tumaini...

error: Content is protected !!