Wednesday , 17 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mbunge alilia barabara ya lami Uwanja wa Ndege Chato
Habari za Siasa

Mbunge alilia barabara ya lami Uwanja wa Ndege Chato

Spread the love

 

MBUNGE wa Biharamulo (CCM), Ezra Chiwelesa, ameiomba Serikali ijenge Barabara ya Nyamirembe-Chato mpaka Katoke Biharamulo , kwa kiwango cha lami, ili kurahisisha usafiri wa kwenda katika Hifadhi ya Taifa Burigi na Uwanja wa Ndege wa Chato, mkoani Geita. Anaripoti Jemima Samwel, DMC…(endelea).

Chiwelesa ametoa ombi hilo leo Jumatano tarehe 26 Mei 2021, katika kipindi cha maswali na majibu, bungeni jijini Dodoma.

“Kwa kuwa barabara hii ni kiunganishi muhimu ambacho kinaunganisha Chato na Biharamulo, kuelekea katika Hifahdi ya Taifa Burigi Chato. Ningetaka kujua muda wa ujenzi utakuwa ni miezi mingapi?” amesema Chiwelesa na kuongeza:

“Pia, kwa kuzingatia umuhimu wa Hifadhi ya Chato Burigi na location ya Uwanja wa Ndege Chato ulipoo, Serikali haioni ni wakati muhimu kujenga barabara hii sambamba na barabara ya Mkingo Chato, ili iweze kuunganisha maeneo hayo ili watu wanaokuja waweze kutoka vizuri?”

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya, amesema wizara hiyo imetenga fedha katika bajeti ya mwaka wa fedha ujao 2021/2022, kwa ajili ya kujenga barabara hiyo.

“Kama nilivyosema katika jibu la msingi, barabara hii imetengewa fedha kwenye bajeti hii na mbunge shahidi. Kipindi cha matengenezo kitagemea na hali halisi ya mazingira, cha msingi ni kwamba mara bajeti ikianza kutekelezwa barabara hii itajengwa,” amesema Mhandisi Kasekenya.

Aidha, Mhandisi Kasekenya amesema kwa sasa wizara hiyo inaikarabati barabara hiyo, ili iweze kupitika.

“Barabara uliyoitaja itaendelea kukarabatiwa katika kiwango cha changarawe, lakini azma ya Serikali ni kujenga kwa kiwango cha lami kadri fedha itakapopatikana. Ili ifike mbuga ya wanyama na Uwanja wa Ndege wa Chato,” amesema Mhandisi Kasekenya.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Samia arejesha mikopo ya 10%, bilioni 227.96 zatengwa

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amerejesha utaratibu wa utoaji mikopo...

Habari za Siasa

Rais Samia amfariji mjane wa Musa Abdulrahman

Spread the loveRais Samia Suluhu Hassan leo Jumanne amempa pole Mwanakheri Mussa...

Habari za Siasa

Nape: Wanasiasa, wanahabari, wafanyabiashara mteteeni Samia

Spread the loveWaziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano,...

Habari za Siasa

CAG: TAWA imegawa vibali vya uwindaji bila idhini ya waziri

Spread the loveRIPOTI ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali...

error: Content is protected !!