Thursday , 2 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kesi za madai, Serikali ya Tanzania yaokoa bilioni 132
Habari za Siasa

Kesi za madai, Serikali ya Tanzania yaokoa bilioni 132

Prof. Palamagamba Kabudi, Waziri wa Katiba na Sheria
Spread the love

 

SERIKALI ya Tanzania, imeokoa Sh.132.24 bilioni, baada ya kushinda kesi mbalimbali za ndani na nje ya nchi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Hayo yamesemwa na Profesa Palamagamba Kabudi, Waziri wa Katiba na Sheria, leo Jumatano, tarehe 28 Aprili 2021, wakati akiwasilisha bajeti ya wizara yake bungenji jijini Dodoma yam waka 2021/22.

Amesema, Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, imeendelea kujenga uwezo wa kitaasisi katika kuratibu, kusimamia na kuendesha mashauri ya madai na usuluhishi kwa kuhakikisha maslahi ya Taifa yanazingatiwa wakati wa uendeshaji wa mashauri hayo.

Profesa Kabudi amesema, katika kipindi cha Julai, 2020 hadi Machi, 2021, ofisi ilianza na mashauri ya madai 3,111 ya kitaifa na kusajili mashauri mapya 545 na kuwa na jumla ya mashauri 3,656.

“Katika kipindi hicho, mashauri 418 yamemalizika na 3,238 yapo katika hatua mbalimbali za usikilizwaji,” amesema Profesa Kabudi.

Amesema, wizara kupitia, Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, ilikuwa na mashauri ya madai ya kimataifa 20, kati ya hayo, mashauri manne yamemalizika na 16 yanaendelea kufanyiwa kazi.

“Katika kuendesha mashauri hayo ya madai ya kitaifa na kimataifa, Serikali imeokoa kiasi cha Sh.132.24 bilioni ambacho kingelipwa kwa wadai endapo Serikali ingeshindwa kesi hizo,” amesema

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza uchaguzi mdogo Jimbo la Kwahani

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi, imetangaza uchaguzi mdogo...

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!