Friday , 29 March 2024
Home Kitengo Maisha Afya Dk. Gwajima: Marufuku kuwauzia kina mama kadi za kliniki
Afya

Dk. Gwajima: Marufuku kuwauzia kina mama kadi za kliniki

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Dorothy Gwajima
Spread the love

 

WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Dorothy Gwajima amepiga marufuku utaratibu wa kuwauzia kadi za kliniki wajawazito. Anaripoti Mwandishi Wetu, Morogoro … (endelea).

Pia, kadi za watoto baada ya kuzaliwa wanapopelekwa kliniki za chanjo kwani ni kinyume na mwongozo wa serikali.

Dk. Gwajima, ametoa maagizo hayo jana Jumanne, tarehe 27 Aprili 2021, mjini Morogoro alipokuwa akizungumza na timu ya wataalamu wa afya, halmashauri na mkoa huo kwenye kikao cha kujadili changamoto za afya ya uzazi, mama na mtoto.

“Nimekua nikipokea malalamiko mengi toka sehemu mbalimbali ya nchi kwamba mama mjamzito au mama akijifungua kadi ya kiliniki wanauziwa kutoka vituo vyetu vya kutolea huduma za afya, hii hapana,” alisema Dk. Gwajima.

Hata hivyo, waziri huyo alisema, amebaini ni kweli kadi hizo zinauzwa jambo ambalo siyo maelekezo ya serikali bali ni utaratibu binafsi wa baadhi ya viongozi wa afya na watumishi wasio na mapenzi mema kwa serikali na wananchi.

Aidha, alisema kufanya hivyo ni kukosa ubunifu na uwezo katika kukabiliana na changamoto za kawaida kabisa mahala pa kazi na hivyo kuwataka watumishi hao kutatua changamoto hiyo kwani gharama za kupata kadi hizo ziko ndani ya uwezo wa halmashauri kitu ambacho wanaweza kuondoa uhaba huo katika maeneo yao bila kusubiri .

Alizitaka pia halmashauri zote nchini, kupata ufumbuzi wa ukosefu wa kadi hizo na asisikie tena malalamiko kutoka kwa akina mama wanaofika kliniki kwani Serikali haitaki kuwaona akina mama wajawazito na watoto chini ya miaka mitano wanapata shida hizo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari Mchanganyiko

Marekani kuipa Tanzania bilioni 980 kudhibiti VVU, UKIMWI

Spread the loveSERIKALI ya Tanzania inatarajiwa kupewa msaada wa fedha kiasi cha...

AfyaHabari Mchanganyiko

Wanavijiji wajenga zahanati kukwepa umbali mrefu kupata huduma

Spread the loveWANAVIJIJI wa Kata ya  Musanja Jimbo la Musoma Vijijini, mkoani...

AfyaTangulizi

Wanasayansi wagundua teknolojia ya kunyofoa VVU kutoka kwenye seli

Spread the loveTIMU ya wanasayansi kutoka Chuo Kikuu cha Amsterdam cha nchini...

Afya

Wananchi 530,000 kufaidika na ujenzi wa hospitali ya bil. 1.8

Spread the love  SERIKALI imetoa Sh 1.8 bilioni kwa ajili ya ujenzi...

error: Content is protected !!