Monday , 6 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa DED Temeke, Sumbawanga wasimamishwa kazi
Habari za SiasaTangulizi

DED Temeke, Sumbawanga wasimamishwa kazi

Spread the love

 

LUSUBILO Mwakabibi, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke na Nyangi Msemakweli, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga, wamesimamishwa kazi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Taarifa ya wakurugenzi hao kusimamishwa kazi imetolewa na Nteghenjwa Hosseah, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano cha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi).

Taarifa hiyo imeeleza Ummy Mwalimu, Waziri wa Tamisemi, amewasimamisha kazi wakurugenzi hao kwa makosa mbalimbali ikiwa ni pamoja na ubadhirifu na usimamizi usioridhisha wa miradi ya maendeleo.

Waziri Ummy Mwalimu

Taarifa hiyo imefafanua, kwamba uamuzi huo umefikiwa baada ya Tamisemi kupokea malalamiko na tuhuma kutoka mbalimbali za wananchi dhidi ya viongozi hao kuhusika na mwenendo wenye mashaka.

Na kwamba, Mwakabibi anatuhumiwa kuhusika na matumizi mabaya ya madaraka, ubadhirifu na usimamizi usiofaa wa miradi ya maendeleo.

Mwakibibi amewahi kuingia kwenye mgogoro na wanahabari kwa muda sasa kwa sababu ya kukataa kutoa taarifa mbalimbali anazoulizwa na siku chache zilizopita, aliamuru kukamatwa kwa waandishi wawili kwa madai waliingia kwenye mkutano wake na wafanyabiashara bila idhini yake.

Taarifa hiyo pia imeeleza, tuhuma zinazomkabili Msemakweli ni ubadhirifu, usimamizi mbovu wa miradi ya maendeleo na uhusiano usioridhisha kati yake na madiwani, Mkuu wa Wilaya na viongozi wengine wa Wilaya na wa Mkoa wa Rukwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Jacob, Malisa wapandishwa kizimbani kwa mashtaka ya uongo mitandaoni

Spread the loveMKURUGENZI wa Shirika la Haki, Godlisten Malisa na mwanachama wa...

BiasharaHabari za Siasa

Bunge laitaka Serikali kudhibiti ufisadi miradi ya mkakati

Spread the loveKAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, imeitaka Serikali kuimarisha...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Wizara ya Uchukuzi yaomba kuongezewa bajeti na Bunge

Spread the loveWIZARA ya Uchukuzi imeliomba Bunge liidhinishe bajeti yake kwa mwaka...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Serikali kutafuta mwekezaji mwingine Bandari ya Dar es Salaam

Spread the loveSERIKALI inaendelea kutafuta mwekezaji mwingine atakayeendesha gati namba nane hadi...

error: Content is protected !!