May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mnyika: Rais Samia amejibu barua ya Mbowe

Rais Samia Suluhu Hassan

Spread the love

 

JOHN Mnyika, Katibu Mkuu wa Chama Kikuu cha Upinzani Tanzania- Chadema amesema, Rais wa nchi hiyo, Samia Suluhu Hassan, amekubali wito wa chama hicho, kukutana na kushauri mambo mbalimbali. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Ni baada ya Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, kuueleza ulimwengu kuwa, wamemwandikia barua Rais Samia ya kuomba kuonana naye.

Mbowe aliyasema hayo tarehe 11 Aprili 2021, alipozungumza na Watanzania kupitia vyombo vya habari, kuhusu mambo kadhaa ikiwemo kifo cha aliyekuwa Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli.

Hayati Magufuli, alifariki dunia tarehe 17 Machi 2021, katika Hospitali ya Mzena, Dar es Salaam na mwili wake, kuzikwa nyumbani kwao Chato mkoani Geita 26 Machi 2021.

Mara baada ya kifo hicho, Samia aliyekuwa makamu wa Rais, aliapishwa kuwa Rais kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania.

Katika maelezo yake Mbowe aliyoyatoa, alisema, Chadema imemwandikia barua Rais Samia ya kuomba kuona naye ili wazungumze masuala mbalimbali yenye manufaa kwa Taifa.

Leo Jumapili, tarehe 25 Aprili 2021, Mnyika kupitia ukurasa wake wa Twitter ameandika, kuwa Rais Samia amewajibu barua hiyo na sasa wanasubiri kupangiwa tarehe.

“Naomba kuwapa taarifa rasmi kuwa tarehe 20 Aprili 2021, tulipokea majibu ya barua ya Mh. Mwenyekiti, Freeman Mbowe ya kuomba kukutana na Mh. Rais Samia Suluhu Hasaa.”

“Rais amekubali kukutana kushauriana na Chadema. Tunasubiri kujulishwa tarehe ya kukutana,” amesema Mnyika

error: Content is protected !!