Wednesday , 8 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Kimbunga JOBO: Usafiri wa anga, baharini wasitishwa
Habari Mchanganyiko

Kimbunga JOBO: Usafiri wa anga, baharini wasitishwa

Spread the love

 

KUFUATIA tishio la Kimbunga JOBO, Ofisi ya Waziri Mkuu imeeleza kusitisha usafiri wa anga, baharini na shughuli mbalimbali kando na ndani ya Bahari ya Hindi. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Hata hivyo, taarifa ya Mamlaka ya Hewa Tanzania (TMA), imeeleza kwamba kadri kimbunga hicho kilivyokuwa kikielekea pwani ya Mafia, kilikuwa kinapoteza nguvu kutokana na kukumbana na upepo kinzani.

Waziri wa Nchi, Ofisi wa Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na watu wenye ulemavu, Jenister Muhagama ameelekeza Kamati za Usimamizi wa Maafa za mikoa, wilaya, kata na vijiji kuchukua tahadhara endapo athari zitatokea.

Muhagama ameagiza menejimenti za maafa ziwashauri wananchi kuhakikisha paa zao zinakuwa imara ikiwa ni pamoja na kukata matawi ya miti iliyopo karibu na nyumba, kufunga milango na madirisha muda wote.

Na kwamba, mambo mengine ambayo kamati hiyo inapaswa kuwashauri wananchi ni pamoja na kuweka akiba ya kutosha ya chakula.

Kwa upande wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), imeelekeza kusimamisha shughuli zote za baharini mpaka hapo taarifa mpya itapotolewa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC, SILABU waungana kufikisha elimu ya fedha majumbani

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeingia makubaliano ya ushirikiano...

AfyaHabari MchanganyikoMakala & Uchambuzi

Kisukari cha mimba ni nini?

Spread the loveKisukari cha mimba ni aina ya kisukari kinachotokea kwa baadhi...

Habari Mchanganyiko

Mafunzo kwa bodaboda 395 yamkuna Meya Dodoma

Spread the loveNAIBU Meya wa Jiji la Dodoma, Asma Karama amepongeza mafunzo...

Habari Mchanganyiko

Samia aagiza huduma za dharura maeneo yaliyoathiriwa na kimbunga Hidaya

Spread the love   RAIS wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Samia...

error: Content is protected !!